Mbunge machachali wa jumbo la Singida mashariki(Ikungi)na mwanasheria mkuu wa CHADEMA Mh. Tundu Lisu jana jioni ametiwa nguvuni na jeshi la polisi mkoani Singida.
Adha hiyo imemkuta Nguli huyo wa sheria na siasa za upinzani nchini baada ya kushuka jukwaani alipokuwa akihutubia wananchi wa Ikungi ambako ndipo makao makuu ya jimbo lake.
Akithibitisha taarifa hizi kutoka ndani ya chama ofisi ya katibu mkuu Bw.Makene anasema Mh.Lisu amekamatwa kwa mile kilichodaiwa ni agizo kutoka makao makuu ya polisi na kwa hvy Lisu atasafirishwa hara iwezekanavyo kwenda Polisi jijini Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni