China imekanusha na kulaani vikali uvumi wa kwamba inazalisha bidhaa nyingi zisizo na ubora stahiki(feki).
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na balozi wa China nchini Tanzania ya kwamba nchi yake kamwe haitengenezi na wala haitatengeneza bidhaa feki,na kwamba bidhaa zote zitokazo china no bora na zenye kudumu.Balozi huyo Bw.Lu Youquing alikwenda mbali na kusisitiza kuwa yeyote mwenye ushahidi na pengine anayo moja ya bidhaa ya Kichina na haina ubora yaani feki basi ampelekee ili naye aione.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni