Hahaahaahaaha,ndiyo tusiishi kwa kulili jamani kwamba mkipishana kauri na mtu basi haiwezitokea mkapatana tena.
Kwa nini msipatane?,pengine dakika moja ya kupatana kwenu inawezakuwa imebeba hatma ya mmoja wenu au hata ninyi nyote.Tumeona hata mitaani kwetu watu walikuwa mahasimu kweli,lkn wakaja kupatana na leo wanatajwa kuwa ni watu waliofanikiwa mno kimaisha.Wakati mwingine hata kwny ndoa,unaweza ona marumbano,ugomvi hata kufukuzana kiasi kwmb unawezasema hawa watu hawatorudiana,lkn cha ajabu wanarudiana na wanafanikiwa.
Ni kweli kwamba kikulacho ki nguoni mwako na rafiki yako ndiye adui yako lkn hayo ni maono binafsi na heshima tunazowapa watu kwa kuamini kuwa wao ni marafiki wazuri na wa kweli.Lkn ktk mpango wa Mungu yule unayemdhani kwamba ndiye adui yako,siku moja anakujakuwa msaada kwako.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni