Jumatatu, 19 Septemba 2016

MAISHA:-TOFAUTISHA NDOTO NA MALENGO

Ndoto Mara chache sana ikawa dhahiri ama yenye ukweli maishani mwa mtu.Ndoto ni kama upepo tu,kwani mtu huweza kuota umelalia mapesa ama umejenga magorofa lkn mara unapoamka tu unajikuta uko vile vile kama ambavyo ulilala yaani huna cha hayo mapesa wala magorofa.
Ndoto husaulika haraka kwani siyo maono ama malengo na wakati mwingine unaweza amka akajikuta umesahau ama hukumbuki vema ulichokuwa ukikiota.Wengi hufa na ndoto zao bila kizitimiza kutokana na ukweli kwamba ndoto huwa haiji na njia,mbinu au hamasa za wewe muotaji kufanikiwa.

Malengo/Maono
~Mara nyingi maono hujenga kitu kwani akionacho MTU NA kukitumainia au kukifanyia kazi ndicho humtafsiri yaani humtokea.
Utafiti unaonesha kwamba waliofanikiwa maishani wengi wao waliongozwa NA kitu malengo ambayo waliyawekeza ktk mile walichokiona ndani yao.
Malengo huleta njia,mbinu na sababu ya kuifanikisha adhima ya MTU ktk maisha.Malengo ni mwanzo wa muundo na udhihirisho wa mtu vile anataka kuwa.Bila maono na malengo ni sawa na kuendesha baiskeli isiyo na breki kwenye mteremko mkali.Bila malengo huwezi hangaikia mafanikio ama kuipangalia na kuitumia vema pesa yako.Bila malengo NA kuichukia hali yako utabaki hivyo hivyo ulivyo.

Hivyo kuna tofauti kubwa sana kati ya ndoto NA maono ama malengo.Anza kuwekeza ktk malengo yako juu ya wewe ni nani na unataka kuwa nani,wakati gani,wapi na kwa nini unataka uwe hivyo.Hii itakufanya kila ulalapo ama uamkapo uikumbuke na kutamani kuitimiza adhima yako.Tunza ama wekeza pesa NA mawazo yako ktk kile unachokiamini na kulenga kukifanya.
Hapa chini tumekuonesha namna ambavyo Vijana wenzetu tayari wameanza kuziishi dhamira zao.Na kwa mtindo huu in dhahiri kwamba kufanikuwa kwao kutakuwa rahisi kutokana na ukweli kwamba tayari wameshakiona NA kukufanyia kazi kile walichokiona ndani mwao NA siyo walichokiota.






Hakuna maoni: