Ijumaa, 19 Agosti 2016

NEWS:-JELA YAMUITA REGNALD MENGI.

Mahakama kuu ya kibiashara ya jijini Dar es Salaam jana imemtumia Bw.Mengi barua ya kumtaka akajieleze mbele ya mahakama hiyo "Kwa nini asifungwe jela kwa kuidharau hukumu ya mahakama hiyo",iliyotolewa Januari 28 mwaka huu kutokana na kesi ya madai iliyokuwa ikimkabili.
Mengi,alishitakiwa mahakamani hapo kwa kesi ya madai iliyoletwa na Bw.Charles Mgweo,Muganyizi Lutagwaba na Erick Mshauli wakimdai Reginald Mengi mabaki yao ya malipo yaliyotokana na Uuzwaji wa hisa wa Kampuni ya Douglas Lake Minerals Ltd ambayo kwa sasa inajulikana kama Handeni Gold Inc...,Mabwana hao kila mmoja wanamdai Mengi 428,750$, 100,000$ na 70,000$ ambayo kwa ujumla wake ni dola 598,750$ ikiwa ni sawa na bilioni 1.2 za hapa Tanzania.

Mbali na Mengi pia jama hao waliishitaki kampuni ya K.M.Prospecting Ltd wakitaka kulipwa ama kumalizia malipo yaliyokuwa yamebakia.
Wito huo wa kujieleza mahakani umekuja baada ya Mengi kushindwa kutekeleza malipo hayo muezi 7 sasa bila sababu mbali na kwamba mahakama ilimtaka afanye hiyo tangu Januari 28...,hali iliyohisiwa na wadai wake kuwa ni dhau kwao na ni dharau mahakama na sheria pia.
Mengi anahitajika kutinga mahakamani hapo mnamo Augost 24 na kujieleza mbele ya jaji wa mahakama hiyo.

Hakuna maoni: