Hakuna aujuaye uchungu wa mwana,malezi na maendeleo yake zaidi ya mzazi.
Kwenye vitabu vya dini tumehusiwa kuwapenda na kuwaheshimu wazazi wetu ili tupate kheri na fanaka maishani mwetu.
Haijalishi hali ya mzazi wako ikoje,iwe kitaaluma,kimaisha au vyovyote vile,daima bado anabaki kuwa mzazi tu na mwenye kustahili kuyafaidi mafanikio yako.
Wazi hutuwazia mema kila kuitwapo leo,hutuombea na kututakua kheri maishani mwetu.Wametulea,wametusomesha hata kutufanikisha ktk maisha yetu.Kumbuka asili yako kwanza kwa kile unachokipata.
Heri yako wewe mzazi wako anaishi hadi leo kuna eenzetu wengine hawana kabisa au hata hawajawahi kuwaona toka wamezaliwa.
Baba na mama walijinyima kwa ajili yako,kuna wakati walukosa usingizi kwa ajili ya afya,taaluma au hata maisha yako yote kuhakikishwa wewe unaishi.
Hebu tujifunze hapa ktk picha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni