Alhamisi, 25 Agosti 2016

UKUTA TU NDIYO SHIDA.

Neno UKUTA yawanyima usingizi wenzetu hasa hawa wanaojiita dola.
Sasa imekuwa shida kila kona kiasi kwamba hata kumuulizia kitu MTU lkn ukataja neno UKUTA lazima kama ulikuwa ukipishana na Askari au mtu asiyependa kusikia UKUTA atageuka kukuangalia.
Jana ktk sehemu mbili tofauti kulitaka kuleta mushkeli.

(1)SINGIDA:-
Jamaa mmoja yuko ktk ujenzi,sasa mida fulani akiwa mjini Mara baada ya kutoka kazini alimpigia simu mkewe ambaye yeye alikuwa eneo la ujenzi(Saiti)akiwasimamia mafundi.Jamaa alizungumza na mkewe vizuri tu lkn katikati ya maongezi akamuuliza hivi,"VIPI MAENDELEO YA UKUTA MMEFIKIA WAPI?"........weeeh kabla hata hajajibiwa alisikia sauti ikimwambia,"AISEE HEBU HIZO HABARI ZA UKUTA ZIFE MARA MOJA".Hapo ilibidi jamaa akate simu na kujitetea kwa kumuelekeza afande kila kitu kuhusu mazungumzo yale.Afande ilimbidi awe mpole.

(2)TANGA:-
Jana Tanga nako kuna jamaa huwa anaprint tisheti.Sasa alikuwa kapewa tends ya kuprint tisheti za kikundi kimoja hivi cha kufa na kuzikana cha mjini humo.Jamaa aliifanya siku hiyo ndani ya Sikh 3 kwa kuwatafutia tisheti zenyewe kwanza ambapo yeye alipendezwa na za ranging nyeusi,akaziprinti kwa maneno yasemayo,"Umoja wa Kuzikana Tanga".
Halafu kwa chini kidoko akaandika kifupi chake yaani UKUTA.Weeeh kazi ikawa ngumu wakati amezipeleka kuwakabidhi wanakikundi.Pamoja NA kwamba Tisheti zilikuwa bomba lkn jamaa walimkatalia kuzipokea wakidai shida siyo gharama au tisheti,Bali shida ni hill neno UKUTA.
Basi fundi akawashauri aongeze neno "M"mwishoni ili isomeke UKUTAM ikimaanisha,"Umoja wa Kuzikana Tanga Mjini".
Weeeeh,wanakikundi wakang'aka unatutakia kifo nini?.Sasa Polisi si watajuwa kuwa UKUTAM maana yake ni Ukuta Mgumu!!!?.
Hakukuwa tena na namna ilibidi tu ile kwa funding maana hats angesema azigawe bure mtaani asingempata wa kuzichukuwa.

Hakuna maoni: