JINSI YA KUKUZA BIASHARA YAKO.
(1)Ongeza idadi ya wateja(Increase the Number of Customers)
Ongeza idadi ya wateja wako kwa kujitangaza.Fanya matangazo kuwafikia watu wengi na kuweza kuongeza wateja kwenye biashara yako.
(2)Ongeza idadi ya mauzo/manunuzi ya kila mteja(Increase the Unit of Sales)
Ikiwa kila mteja anakuingizia wastani wa shilingi elfu 10 tu kwa kila manunuzi yake;inakulazimu ujitahidi kumshawishi mteja huyo anunue na bidhaa zingine za ziada ambazo zitakufanya uongeze mapato yako kwa kila manunuzi yake kwako.
Mfano:-
KFC na McDonald hasa ni hodari sana katika hilo.Kwao ukiweka oda ya burger;watakuuliza ,"He,utapenda tukuwekee na chipsi?".Ukisema ndiyo pia watakuuliza tena,"Utapenda tukuwekee na kinywaji gani?".
Hivyo hapo utakuta lengo la mteja nilikuwa anunue burger lakini watajikuta wameuza chipsi na kinywaji zaidi kwa mteja wao.
(4)Ongeza Unafuu,Ubora na Uhakika wa bidhaa ama huduma yako.
Ujitahidi sana kuwa tofauti na wengine kwa kuongeza Unafuu wa gharama kwenye bidhaa ama huduma yako.Pia hakikisha unakuwa na bidhaa au huduma bora na zenye Uhakika wa upatikanaji wake kila zinapohitajika.
Mfano:-
Kuwa na mawasiliano mazuri na wale wanaokuuzia mzigo wa jumla ili kujuwa ingizo jipya la mzigo mpya ili uwe wa kwanza kupata bidhaa hizo kabla ya wengine unao chuana nao kibiashara.
(5)Uwe muaminifu.
Jenga uaminifu kwa wateja wako.Jenga uaminifu kwa jamii yako na lakini pia kuwa muaminifu kwa kipato kitokanacho na biashara yako.Kuwa muaminifu hata kwa wale wanaokusaidia kazi na majukumu mengine kwenye biashara yako.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni