Na Joachim L.Mkwawa
Sabuni ya mche unawezaitumia kufulia,kuogea ama kuoshea vyombo nk.
Namna ya kutengeneza sabuni ya mche.
MALIGHAFI:-
(1)Mafuta ya Mbosa/mawese/Nazi Lita 4.
(2)Maji mililita 350×4=1400;ambazo ni sawa chupa 4 za soda zilizojaa vizuri.
(3)Caustic Soda 0.5kg
(4)Sodash 0.5 kikombe cha chai.
(5)Perfume.
(6)Box.
JINSI YA KUTENGENEZA:
Zingatia hatua zifuatazo pamoja na vipimo kama ninavyoelekeza ili utengeneze kitu bora,salama na chenye uhakika sokoni.
(1)Loweka Caustic Soda 0.5kg kwenye maji mililita 1400.
~Koroga na uifunike.Uache mkorogo huo ulale Massa 24 had I kesho.
(2)Kesho yake pasha moto mafuta.
~Ipua acha yapoe ibakie joto kiasi.
~Kisha yamimine mafuta hayo kwenye chombo kingine cha plastiki.
(3)Chukua Caustic Soda uliyoikoroga jana imimine kidogo kidogo kwenye chombo kile cha plastiki ulichoweka mafuta; huku ukikoroga haraka haraka kuelekea upande mmoja.
(4)Baada ya hapo koroga Sodash kwenye chombo kingine,kisha imimine kwenye mchanganyiko wa Caustic Soda na Mafuta huku ukiendelea kukoroga kuelekea upande mmoja.
(5)Weka perfume vijiko 2 vya chakula kisha koroga hadi uji uji use raini kabisa.
(6)Andaa box;mimina mkorogo huo ndani ya box.Acha ilale humor hadi kesho yake.
(7)Baada ya hapo utakata vipande vipande uvitakavyo wewe na Sabuni yako ya mche itakuwa tayari kwa matumizi.
Kwa maelezo zaidi ama kujifunza kwa vitendo tafadhali wasiliana nami kupitia +255 625887699 au +255 710590088.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni