Jumatano, 10 Agosti 2016

VIJANA NA MAISHA.

MADA:-ITAKUWAJE?
Ktk maisha ya sasa,vijana wengi tunateswa sn na muonekano wa mambo kwa nje tu.Hofu yetu huletwa na swali lisemalo ITAKUWAJE?
Itakuwaje km nitachukuwa hatua ya kutoka ktk mazingira niliyozaliwa,nikalelewa na kukulia ama mahali nilipopazoea na kufahamika na kila mtu halafu nikatafute maisha sehemu ya mbali?,huko siyo kwetu,sina anayenifahamu na wala spajui vema?.
Au Itakuwaje km nitatumia kiasi hiki cha pesa kununulia kiwanja halafu ghara za kujengea nyumba ntazimudu?.,Itakuwaje kama nikiamua kutoka nyumbani ili nikajitemee kivyangu kwa kupanga chumba?,ntawezaje kuzimudu gharama za maisha?,itakuwaje iwapo ntakosa pesa ya pango,bili ya maji,umeme,au kulupia king'amuzi?,au endapo ntakuwa na mke itakuwaje siku nikikosa pesa ya kugharamia maisha na mahitaji yote ya nyumba NA familia?
Itakuwaje endapo ntakosa kazi ya kufanya huko halafu no ugenini?Hapana kheri nibaki tu hapa hapa nyumbani maana in salama.
Hali hii imetukwamisha sana kimaisha wengi wetu.Tumekuwa waoga Dana wa kuthubutu kutenda jambo,huku tunajipa moyo kuwa kheri tuishi tu mazingira tuliyazoea.Tunasahau yote ni mipango tu ya Mungu na juhudi binafsi ndivyo vyenye kumfanikisha yeyote yule msishani.
ITAKUWAJE?-Ni njia na ni hisia tu za kimwili na nafsi ambavyo kwa kawaida huzipinga haja za roho ya mtu.Roho daima inawaza ushindi NA ndiyo kusudi LA kuumbwa kwake.Ndugu na kijana mwenzangu tambuwa kuwa uliumbwa kuwa mkuu,uliumbwa kushinda,uliumbwa kuiongoza Dunia.Hebu jiulize Duniani tupo wanadamu zaidi ya bilioni 7,je ukiondoa wewe hao waliobaki wanalishwa NA kuvishwa na nani?.Akilini mwako ondoa hilo wazo potofu LA kwamba ITSKUWAJE?.Gundua karama yako,changanua mazingira yako,Chukua hatua ukianza na kile ulichonacho.Itakuwaje itakufelisha maisha.
Binafsi nilikuwa mlevi wa kutupwa,nilipoteza pesa NA muda wangu mwingi ktk ulevi.Nilitamani kuachana nayo kwa sabsbu tu ya adha yake lkn swali itakuwaje nikiachana nayo nitaishi kweli.Ila siku moja pombe ilinifedhesha Mno NATO ilikuwa May 5 2015 nikawa hatarini kufa NA kupoteza kazi lkn n
 Nliamua na kujisemea Ee Mungu nisaidie maana naiona kesho yng.Kisha nikaamuua kusema baaasi inatosha.Sikufichi had I Leo Nina miaka 3 situmii tens pombe.Nimeweza kujikwamuwa kimsisha.ITSKUWAJE? Ingeweza kunikatisha tamaa ningefika hapa?,ama ningeyaruhusu mawazo ya kusema itakuwaje wenzangu watakapokuwa wanakunywa halafu mm sinywi,je itakuwaje vile pombe ilivyotawala na kuamini bila hiyo mm ntawezaje kuishi?.
Inawezekana kabisa nilichukiwa NA kutengwa NA wenzangu lkn ckujali.Hv Leo nimefanikiwa ingawa ilikuwa ngumu.Hivi uliwahi jiuliza kwamba Mwl.Nyerere angeliruhusu swali ITAKUWAJE angeikomboa Tanzania toka kwa wakoloni?,Gabo Zagamba angejihoji na kuogopa kupambana ktk tasnia ya filamu nchini akihofia akina Ray na wengineo angefika hapo alipo?Ujasili huleta utajiri.Usikate tamaa,ushindi wetu upo mikononi mwetu.





Hakuna maoni: