Tukio la kinyama limetokea muda huu saa 19:30 pm ktk maeneo ya benki ya Mmbande baada ya watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi kutaka kuvamia benki hiyo na kutoka na pesa kukwama na kutimuka huku wakiacha wameuwa askari 3 wa jeshi la polisi.
Majambazi hayo yalishindwa kuvunja benki hiyo baada ya kushitukiwa na askari hso ambao mmoja alikuwa anatoka lindoni na mwingine akiwa anaingia kumpokea mwenzie na mmoja mwingine akiwa ni dereva aliyemleta mwenzie.
Askari walokufa ni
(1)E5761 CPL Yahaya
(2)F4660 CPL Hatibu na
(3)G9544 PC Tito.
Hata hivyo mbali na kutekeleza mauaji hayo,majambazi hao walokuwa na pikipiki watokomea kuelekea Mvutin huku wakifanikiwa kukimbia na SMG moja mali ya jeshi la polisi.
Habari na chanzo chetiu
Johnson Kahwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni