Leo tunaangazia tabia za waendesha vyombo vya moto ambavyo hawatii sheria.
Sheria za usalama barabarani ziko wazi tu na zinazungumzwa na kusimamiwa kila uchwao ili zitekelezwe lkn mtu na hakili zake kwa makusudi anazivunja sheria hizi.Kwanza aliyekitengeneza chombo hicho cha usafiri pamoja na ujuzi wote alonao,bado alikumbuka kuweka kiwango cha mwisho cha uzito wa mzigo ufaao kupakiwa na chombo hicho.Sheria nazo zikawekwa ili kutilia mkazo ktk kudhibiti matumizi sahihi kwanza ya barabara,kisha ya vyombo vyenyewe vya usafiri lkn pia na usalama wa watumiaji wote wa barabara.
Mtu kama huyu,amejaza mzigo namna hii,hivi hata mbele anaona kweli,je anaona nyuma?.Huyu akishurutishwa kwa kosa hili atakuwa kaonewa?.Mwanausalama gani wa barabarani asiyejipenda akutane na wewe unayafanya haya halafu akuache?.
Aaah....MPIGWE TU MAANA MNAJITAKIA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni