Akiwa ktk ziara yake jana jijini Mwanza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli alisema kwamba serikali yake ya awamu ya tano imedhamiria kuibadili Tanzania na kwamba itajenga viwanda vingi vya nguo hapa nchini ili Watanzania wavae hadi wasaze na baada ya nguo hizo kuvaliwa na kuchoka basi itakusanywa na kupelekwa kuuza tena Ulaya kama mitumba.Aluongeza kuwa hataki kuona Watanzania wanaendelea kuvaa nguo zilizokwisha kuvaliwa(mitumba)ambazo zinavaliwa na kisha zinaletwa na kuuzwa tena Tanzania."Ifike wakati Watanzania tuamue kuzalisha vya kwetu na tuvitumie vya kwetu ili na sisi tupate masoko kwao".,Alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni