Na Joachim Mkwawa.
Karibu tena ndugu msomaji na mjasiriamali mwenzangu katika dawati hili La UJASIRI NI MALI(JIAJIRI)ili uchote maarifa.
Na Leo nataka ujifunze KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI.
Sabuni hii ya MAJI unaweza itumia kudekia ndani kwako(nyumbani),kufulia au kama utataka kuitumia kwa ajili ya kusafishia maliwatoni(choo na bafu)Basi huna budi kuongeza kiwango cha perfume kidogo wakati wa kuitengeneza.
Hebu ungana nami hapa chini hatua kwa hatua ujuwe.
MAHITAJI/MALIGHAFI:-
(1)Salfoniki asidi nusu lita.
(2)Slees robo kg
(3)Sodash robo kg
(4)Maji lita 15
(5)Rangi nusu kijiko
(6)Sodiamu salfeti nusu kg
(7)Perfume vijiko 2
(8)Formaline vijiko 2
(9)Glyceline vijiko 4.
JINSI YA KUTENGENEZA.
(1)Andaa Diaba(jana)au chombo chochote cha ujazo wa lita 20.
(2)Weka Maji kiasi kwenye chombo chako.Hakikisha chombo chako ni kikubwa na kina ujazo unaozidi wingi wa Maji yako.
(3)Weka Salfoniki Asidi,Slees koroga kisha weka Maji tena na uendelee kukoroga kuelekea upande mmoja.Yaani unakoroga kuelekea kulia usigeuze kuelekea kushoto.
(4)Weka Sodash,Rangi uipendayo,Perfume, Formaline na Glyceline kisha endelea kukoroga mchanganyiko huo kwa dakika 2 au 3.
(5)Chukua chombo kingine cha plastiki mfano jagi au bakuli,chota huo mchanganyiko wako kiasi kupitia jagi au bakuli kisha chukua sodiamu tia kwenye hill jaki au bakuli lenye mchanganyiko uliyouchota toka kwenye jaba;halafu koroga ili sodiamu ichanganyike vizuri.Baada ya hapo mimina huo mchanganyiko wa kwenye bakuli au jagi umiminie kwenye ule mchanganyiko mwingi wa awali uliyomo kwenye jaba na uendelee tu kukoroga ndani ya jaba huku unaumimina mkorogo uliyomo kwenye bakuli au jagi.
Na hapo utaanza kuona mkorogo/mchanganyiko wako unaanza kupanda(kuongezeka/kuumuka)kuja juu.Kwa nini inakuwa hivyo??.
Ni kwa sababu Sodiamu huongeza wingi wa sabuni yako.Hivyo ukikoroga lita 15 hakikisha chombo chako kiwe kina ujazo wa lita 20 au zaidi.
Formaline husaidia kuitunza sabuni yako isiharibike haraka;yaani ukiweka Formaline basi sabuni yako inaweza kaa hata mwaka 1 bila kuharibika.
Ukimaliza,weka sabuni yako kwenye vifungashio(parkeg) tayari kwa biashara na matumizi.
KUMBUKA:-
Kuna aina 5 za Formaline.
(1)Formaline ya Chakula.
(2)Formaline ya Dawa.
(3)Formaline ya Sabuni.
(4)Formaline ya Maiti.
(5)Formaline ya kuzuia wadudu wasiharibu lotion.
Hivyo kuwa makini sana wakati wa kununua Formaline kulingana na uhitaji wako ama unakwenda kuitumia kufanyia nini.
MALIGHAFI zote hizo zipo na zinapatikana kwenye maduka maalum ya wajasiriamali nchi nzima.
Ukizingatia na kufuata vema hatua hizo hapo juu utakuwa hodari sana na mzalishaji mkubwa wa sabuni hii ya Maji.
Ahsante.
Wako ktk ujenzi wa Taifa
Joachim Mkwawa
Email:-joachimmkwawa8@gmail.com
Call/WhatsApp +255 625887699.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni