Jumanne, 13 Septemba 2016

UPENDO NI TIBA KWA NAFSI ILIYOJERUHIWA.

Upendo ni nini?
~Ile hali yenye udhihirisho wa uthamini,kujali,kusaidia,kuvumilia,kujitolea.Upendo huokoa maisha,Upendo huhamasisha na kudumisha Amani.Upendo hutibu na kuponya jeraha la nafsi,lkn pia Upendo husahaulisha maumivu.
Mwenye Upendo haoni hasara kujitolea kwa ajili ya wengine,mwenye upendo hatarajii sana faida kwa hisani yake kwa yule anayemuhisani.Ktk Upendo kuna Amani na hivyo kuna mapatano yenye tija ama maendeleo.Upendo ni kujitoa mhanga kwa ajili ya mwingine.Upendo ni udhihitisho wa kutaka wengine waishi wakijuwa na kuamini kwamba wanathaminiwa hata kwa hali zao duni ama udhsifu wao.
Tumeagizwa Upendo hvy yatupasa tupendane.Na ili tudumu ktk pendo hatuna budi kuvumiliana na kusameheana pamoja NA kuombeana kheri ktk madhaifu yetu...maana Upendo huvunja matabaka.Tusiwe na Upendo wa kinafiki maana unafiki ktk pendo hujeruhi nafsi,matarajio au mipango na hatima za wengine maishani.

Hakuna maoni: