Jumatano, 10 Agosti 2016

TUME YA MAADILI YAUMBUKA.

Tume ya maadili ya utumishi wa umma nchini yaumbuka.Kuumbuka huko kumekuja baada ya Kamishina wake mkuu jaji Salome Kaganda kukanusha uwepo wa barua za uvunjifu wa maadili ya utumishi wa umma ambazo ziliandikwa na kutumiwa mwanasheria mkuu wa Chadema  Tundu Lisu na m/kiti  wa Chadema taifa mh.Mbowe kwamba wajieleze kwa mini wasichukuliwe hatua za kisheria kutokana na kukiuka viapo vyao.Barua hizo ambazo zinaonesha wazi zilitoka ofisini mwa mama huyo hatimaye leo jaji Kaganda amedai yeye hajui kama kuna uwepo wa barua hizo na kwamba inalenga kumchafua.
Hayo yamekuja Leo baada ya mh.Lisu kuzungumza hadharani na waandishi wa habari kuhusu barua hizo,UKUTA pamoja na ufanikishaji wa oparesheni UKUTA ilopangwa kufanyika Sept mosi mwaka huu nxhini kote.
Chanzo chetu cha habari hii kinadai kuwa uwepo wa barua hizo na taarifa ya ukanushaji wa jaji Kaganda kuandika barua hizo kunalenga kuvunja uhusiano uliopo kati ya Chadema na jamii ya Watanzania wapenda haki na kwamba inalenga kuikandamiza Chadema.Chanzo hicho kilikwenda mbali na kudai kuwa sheria ya nchi iko wazi na inawapa wapinzani wa kisiasa kama chama kufanya wanachotaka kufanya ikiwemo kuikosoa serikali au kuishauri au kuipongeza endapo tu imefanya vizuri ikiwa ni pamoja na kufanya mikutano,makongamano au maandamano ya Amani ili kuvuna wanachama wapya kwa kueneza au kutangaza na kunadi Sera zao tofauti na ilivyo sasa ambapo wanakatazwa na kila anayeonekana hata kofia tu ya Chadema ni shida.


Hakuna maoni: