Mzazi ni mzazi tu hata aweje,wengi wetu leo tukiona tuna angalau unafuu wa msisha basi tunsahau mwanzo wetu,hatujui kuwa hata ktk kufanikiwa kwetu wazazi wamechangia kwa kiwango kikubwa na cha pekee sana,wakati mwingine walifanya kazi za kuwadharirisha ili tu ww usome,ule,uvae na hasa kukufanya usijutie maisha yako.Kuna wakati mzazi anafunga na kuomba au anaraluka hadi mavazi,hatamaniki kumuangalia ili tu wewe ufanikiwe lkn mwishowe tunasahau.
Hata iweje mzazi ni sehemu ya furaha yako,mzazi amewekeza kwako anataraji msvuno na hiyo haina mjadala kwani ni haki kwake na ni wajibu kwako kumuinua.
Hakuna atakayelia zaidi pale wewe ukiumia zaidi ya mzazi wako
Vitabu vya Mungu pia vimetuasa tuwapende baba na mama zetu ili tupate kheri na baraka maishani.Hujachelewa anza sasa,mkumbuke baba,mkumbuke mama hata kwa maombi utaona na kupokea majawabu juu ya changamoto zako na utafanikiwa maishani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni