Alhamisi, 18 Agosti 2016

KUPIGWA TUNAJITAKIA

Unajuwa mara nyingi mtu huwezi pigwa,kutapeliwa au hata kupoteza muda wako kukiuka taratibu zilizowekwa na ndiyo maana unashauriwa kwamba uliza pale unapoona hupaelewi ili yasikukute ya kukukuta.
Dada huyu kama anavyoonekana alitoka atokako na kuja kununua nguo kwny duka flani hivi.Cha kushangaza zaidi baada ya kufika nje ya duka akakuta kuna kama watu wamepanga foreni hivi kuelekea ndani.Sasa naye bila kuchunguza akajikuta anapanga foreni hiyo,Jamaani alisimama hadi akachoka,muda ukazidi kwenda foreni haiishi.Alitamani kuuliza lkn akaogopa,punde kuna kijana alitoka nje ya duka hilo na haraka haraka yule dada akaona bora aulize.Ikawa hivi:
Dada:Sorry kaka,eti humo ndani watu wengi sana?
Kaka:Mh hapana mbona nipo mwenyewe tu na ndiye muuzaji,vipi kwani?
Dada:Aah,tumepanga mstari muda mrefu hatuoni dalili za kuhudumiwa.
Kaka:Hahaahaaahaahahaa,Duh!,dada mbona umepanga foreni na masanamu.Kwa kukuhakikishia ngoja nilitingishe moja ujionee.Alivyolitingisha likadondoka.
Je,unajuwa kilitokea nini?,miye simo.
Mtu kama huyo kwa nini asilizwe,asitapeliwe?
KUPIGWA TUNAJITAKIA.

Hakuna maoni: