Ijumaa, 5 Agosti 2016

ML.10 YAMCHOMOA LISU RUMANDE.

Hatimaye Mwanasiasa na mwanasheria nguli wa CHADEMA Bw.Tundu Lisu(Mp)ameachiwa kwa dhamana na mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.Dhamana hiyo imekuja pale ambapo mahakama hiyo imetupilia mbali madai ya kupingwa kwa dhamana dhidi ya Mbunge huyo wa Singida Mashariki kwa kile kilichodai hakuwa na haki ya kudhaminiwa kutokana na mashtaka yanayomkabili.
Lisu alitiwa nguvuni juzi mjini Ikungi mkoani Singida mara tu baada ya kushuka toka jukwaani alipokuwa akihutubia mkutano kwa wananchi wa jimboni kwake kwa kile kilichodaiwa kuwa ni agizo kutoka makao makuu ya polisi jijini Da es Salaam.
Hata hivyo CHADEMA imelaani vikali na kulitupia lawama jeshi la polisi kwamba linatumika vibaya ktk kuchangia ukandamizwaji wa demokrasia nchini.Lisu alichukuliwa Ikungi,akapelekwa Singida mjini NA haraka sana alifikishwa Dar es Salaam na kuhojiwa usiku kucha ambapo inakadiriwa kugharimu Massa 23.Baada ya Lisu kufikishwa mahakamani Kisutu,hatimaye Mahakama ikalitupilia mbali dai la polisi la kumnyima dhamana,na kwa hvy Lisu akachiwa na mahakama kwa dhamana ya Taslimu shilingi Ml.10 za Kitanzania.

Hakuna maoni: