Hatimaye Mgombea Ubunge na mshindi wa pili ktk uchaguzi mdogo uliofanyika Disemba 2015 huko Masasi-Mtwara afariki Dunia.
Mgombea Hugo ambaye no Ismail Issa Makombe a.k.a Baba Kundambanda aligombea nafasi hiyo kupitia CUF na UKAWA akiziba pengo la aliyekuwa mgombea wa awali Mh.Emmanuel Makaidi ambaye naye alifariki kabla ya uchaguzi mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani ulofanyika Oktoba 2015 akiwakilisha chama cha NLD na UKAWA kwa ujumla.
Mwanasiasa huyo ambaye pia alikuwa ni Msanii wa vichekesho ktk kundi la Vituko show ktk uchaguzi mdogo wa Disemba 2015 yaani mwaka jana alishika nafasi ya pili nyuma ya mpinzani wake kutoka CCM Mh.Rashid Chua Chua.Ambapo marehemu alipata kura 14,069 akimfuatia mshindi wa uchaguzi huo aliyepata kura 16,597.
Mheshimiwa na Msanii Baba Kundambanda atakumbukwa an has a ktk tasnia ya filamu hapa Nchini akiwakilia Komedi kupitia vituko na rafudhi yake ya wenyeji wa Mtwara.Taratibu za mazishi zinaendelea huko nyumbani kwao Masasi Mtwara.
Mungu alitoa na Mungu ametwaa.Jina lake lihimidiwe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni