Jumapili, 17 Julai 2016
MICHEZO:Hatimaye Shule ya Sekondari Chamwino iliyoko Chamwino-Ikulu ambapo ni makao makuu ya Wilaya ya Chamwino yajipatia kiwanja safi na kipya cha mpira wa kikapu.Akizungumza nasi Mwl.Stephane Lemwai ambaye pia ndiye Mkuu wa shule hiyo amethibitisha kwamba kiwanja hicho ni kweli kimepatikana na kutengenezwa ktk ubora wa aina yake.Hvy sasa Wanafunzi na wapenzi wa mchezo huo watarajie mambo mazuri na timu bora ya mchezo huo kutoka shuleni hapo.Lkn pia amesisitiza kuwa wadau wote wa michezo pamoja na wanafunzi wote wajitokeze kuusapoti mchezo huo ikiwa ni pamoja na kuutunza na kuulinda uwanja huo ili udumu pamoja na kuzalisha vipaji vingi zaidi kupitia mchezo huo.Kila lakheri Mwl.Stephane Lemwai,walimu,bodi ya shule pamoja na wadau woote bila kusahau jamii ya Wanachamwino ktk kuendeleza michezo na kukuza vipaji mjini Chamwino.

Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni