Jumatano, 27 Julai 2016

CHADEMA YAKANUSHA KIFO CHA NDESAMBURO

Chama cha Demokrasia na Maendeleo nchini CHADEMA kimekanusha uvumi wa taarifa zinazozidi kuenea mitandaoni kwamba Mbunge msaafu wa jimbo la Moshi mjini na M/kiti wa chama hicho Mkoani Kilimanjaro Mh.Ndesamburo kuwa ameaga Dunia usiku wa kuamkia leo kuwa Habari hizo ni za uongo.
Kupitia chanzo chetu cha Habari hii,ni kwamba Mh.Ndesamburo ni mzima kabisa wa afya akiendelea na shughuli zake za kila siku.Akizungumza kwa kujiamini ndugu Basili Lema amesema taarifa hzo potofu si za kutiliwa maanani kwani zinalenga kuupotosha umma na hasa wanachama wa chama hicho kuendelea na mambo ya msingi badala yake waanze kukimbizana na tukio hilo lisilo na ukweli.Hata hivyo amelaani vikali kwa wote wale wanaoendelea kuueneza uongo huo na kudai kuwa ni watu wabaya wasiyoitakia mema CHADEMA na hvy hawafai Hata kutazamwa usoni.

Hakuna maoni: