Jumamosi, 30 Julai 2016

MAJENGO YA SERIKALI DAR KUPIGWA MNADA.

Baada ya Mh.Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli kuitaka Serikali yake kuhamia Dodoma ambako kikatiba ndiyo makao makuu ya Tanzania,Mawaziri,na watendaji wengine tayari kuanza harakati za kuhamia Dodoma,jana Rais Magufuli amesema kuwa Majengo yote yaliyokuwa ya Serikali atayapiga bei na pesa itakayopatikana itatumika kuujenga mji wa Dodoma.
Magufuli aliyasema hayo jana alipokuwa mkoani Singida ktk ziara yake ya kikazi ya siku nne ikianzia Singida,Tabora,Shinyanga na Geita.Akizungumza na Wananchi Magufuli alisema amedhamiria kuifanya Dodoma kuwa Makao makuu ya nchi kivitendo,huku akiwataka wananchi kufanya kazi kwa bidii badala ya kujihusisha na mijadala au maandamano yanayoashiria kupinga juhudi za Serikali kuwaletea wananchi maendeleo.


Hakuna maoni: