Jumapili, 17 Julai 2016

CHOBO INVESTIMENT YAHAMASISHA VIJANA KTK UWEKEZAJI.

Kampuni ya uchakataji nyama jijini Mwanza iitwayo Chopo Investiment yawa kivutio na kichocheo cha vijana kuhamasika kujiajiri kupitia uwekezaji binafsi badala ya kusubiri kuajiriwa ama kushinda vijiweni.Mradi huo ambao unamilikiwa na kijana mzawa Mtanzania Bw.John Chobo umekuwa kivutio kikubwa cha uwekezaji kupitia rasilimali na mazingira yanayotuzunguka.Akizungumza pindi mradi huo ulipotembelewa na Mh. Waziri anayeshughulikia ajira na vijana Mh. Anthony Mavunde,Bw.Chobo anasema Mradi huo wenye machinjio za kisasa na mashine maalum za kuchakatia nyama umegharimu zaidi ya Tsh.8ml,na kwamba tayar hadi sasa umeajiri Wanamwanza 200 lkn pia anaongeza kuwa mradi huo utakapokamilika utaweza kuwaajili vijana zaidi ya elfu 1.Hili ni somo kwetu vijana,tuache uzembe badala yake tuumize vichwa tugundue nini cha kufanya kujipatia kipato.








Hakuna maoni: