Jumapili, 17 Julai 2016

MICHEZO:Hatimaye usiku wa tarehe 17/7/2016 wakamilisha ligi kuu ya Vodacom kwa hapa bara kwa Shirikisho la soka bara TFF kutangaza na kukabidhi tuzo kwa washindi mbalimbali wa ligi hiyo.Ktk hafla hiyo ambayo imehudhuriwa pia na Waziri wa mambo ya ndani Mh.Mwigulu Lameck Nchemba pamoja wageni wengine waalikwa imeshuhudia Timu,makocha,wacheza na Marefa wakijinyakulia zawadi zao.Ambapo kwa mhutasari ni kwamba washindi Young Africans wamejinyakulia Tsh.81ml,huku mchezaji bora,mfungaji bora,kocha bora wote wakitokea Yanga.Huku timu ya pili ambao ni Azam FC wakijinyakulia Tsh.40ml na timu ya Simba SC zote za Dar es Salaam nayo ikijishindia Tsh.27ml huku timu ya nne ikiambulia Tsh.23ml.Pia tuzo hizo zimeshuhudia kipa bora akitokea Simba,mchezi bora wa kigeni akitokea Yanga huku mchezaji timu yenye nidhamu nayo ikitokea pamoja na Mwamuzi bora wa ligi hiyo naye akihinyakulia kitita chake.Kukamilika kwa hafla hiyo kuna ashilia kwamba ndiyo mwanzo wa maandalizi ya msimu mwingine wa ligi hiyo kuanza tena kutimua vumbi hivi karibuni.Hata hvyo Utani wa jadi nao haukuwa nyuma kama inavyoonekana ktk picha.

Hakuna maoni: