Jumapili, 17 Julai 2016

MAKALA:MAISHA YANAYOONGOZWA NA MALENGO

Habari za leo mdau na msomaji wetu wa Blog hii.Awali ya yote napenda kuwadhukuru nyote kwa kutembelea na kujifunza mengi kupitia hii Blog yetu.
Leo napenda tujifunze kuhusu Maisha hasa Maisha yanayoongozwa na Malengo.
Maisha ni neno lenye maana nyingi kulingana na vile mtu anavyoyaona,kuyachukulia na kuyaishi maisha.Lakini Maisha ni ile hali ya kuwa hai.Hvy ni mjumuiko wa vitu kuwa ktk hali ya uhai.
Hivyo ili kuendelea na kudumu ktk uhai kunategemea mambo mengi ikiwemo
-Afya
-Maji
-Chakula
-Makazi
-Mazingira
-Kipato nk.
Sasa basi ili kuvipata vitu hvy nguvu,akili,juhudi na ushirikishwa vinahitajika.
Maisha yayoongozwa na Malengo ni Kuyaona maisha ktk njia za Kiungu.Hapa ni pamoja na:-
(1)Kulijuwa kusudi la kuumbwa kwako(Gundua Karama yako)
(2)Changanua Mazingira yako,kwamba yanafaa kwa kile utakachokiendesha na kukufanikisha ukaishi?
(3)Anza na kidogo ulicho nacho.Kumbuka Mungu anaheshimu mwanzo mdogo.Hvy anza na mtaji kidogo ulo nao,uzalishe na kuuendeleza.
(4)Jirekebishe ktk matumizi yaani punguza mstumizi ktk vitu unavyovipenda hasa vya anasa.
(5)Wekeza pesa yako mara nyingi zaidi ktk kile kikupacho faida.
(6)Ukubali kukosolewa na kuchukuwa hatua za kujirekebisha pale unapokuwa umekosea.Hii itakuboresha zaidi.
(7)Epuka au punguza marafiki wasiofsa kwsko na ruhusu akili yako kujifunza sma kuambatana na waliofanikiwa.
Kwa leo tuishie hapa.Maisha ya sasa ni magumu na yanahitaji sana akili na kujituma bila kusahau kutokuchagua kazi na pia kujitahidi kuibua na kuzitendea haki fursa unazokutana nazo ili mradi tu zs halali.
Ahsante,
           Wako
                   Joachim Mkwawa 0629114323


Hakuna maoni: