Hatimaye maandalizi pamoja na mipango ya CCM,kwa ajili ya mkutano wake mkuu ambao unatarajiwa kufanyika mnamo 23/07/2016 inaendelea kukamilika ambapo tayari Bendera za taifa na za chama zimeanza kupepea.
Hii inamaanisha CCM iko tayari kwa mkutano wake huo ambao utahudhuriwa na wajumbe wake 2000 ili kupiga kura za ndiyo kumchagua M/kiti wake wa chama taifa.Pia shughuli hiyo itashuhudia Rais mstaafu wa awamu ya nne Mh.Dkt Jakaya Kikwete ambaye ndiye M/kiti wa sasa anayemaliza muda wake akimkabidhi kijiti au kiti hicho M/kiti mpya wa chama hicho kikubwa na kikongwe kunako Siasa hapa Nchini Mh.Dkt John Pombe Magufuli.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni