Jumapili, 31 Julai 2016

MAPACHA WASABABISHA KIFO CHA BABA YAO.

Mwanaume mmoja Afrika kusini ajiua kwa kujiteketeza kwa moto hadi kufa baada ya mkewe kujifungua mapacha wenye asili ya Kuchina.
Habari zinasema mwanamama huyo alikuwa akifanya kazi kwny mgahawa wa Wachina,hvy yaweza kuwa alipata mimba toka kwa mmoja kati ya mabosi wake hao.

WAZO LA LEO


MCHANA NA KATUNI

Ni pale baba anapoitelekeza familia au kuwa mbinafsi.

Jumamosi, 30 Julai 2016

WAZO LA LEO


MCHANA NA KATUNI

Leo tunaangazia mahusiano ya mastar wa bongo na umri wao ambapo Mastar wa kike wana umri mkubwa zaidi ya wapenzi wao wa kiume ambao kimsingi ni wadogo kiumri.

MAJENGO YA SERIKALI DAR KUPIGWA MNADA.

Baada ya Mh.Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli kuitaka Serikali yake kuhamia Dodoma ambako kikatiba ndiyo makao makuu ya Tanzania,Mawaziri,na watendaji wengine tayari kuanza harakati za kuhamia Dodoma,jana Rais Magufuli amesema kuwa Majengo yote yaliyokuwa ya Serikali atayapiga bei na pesa itakayopatikana itatumika kuujenga mji wa Dodoma.
Magufuli aliyasema hayo jana alipokuwa mkoani Singida ktk ziara yake ya kikazi ya siku nne ikianzia Singida,Tabora,Shinyanga na Geita.Akizungumza na Wananchi Magufuli alisema amedhamiria kuifanya Dodoma kuwa Makao makuu ya nchi kivitendo,huku akiwataka wananchi kufanya kazi kwa bidii badala ya kujihusisha na mijadala au maandamano yanayoashiria kupinga juhudi za Serikali kuwaletea wananchi maendeleo.


Ijumaa, 29 Julai 2016

KUFANANA NA RAIS KWAZUA TAFLANI DAR.

Leo ktk mitaa ya soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam,kumetokea taflani baada ya mtu mmoja anayesadikiwa kufanana kwa sura na Rais Dk.John Pombe Magufuli kutinga sokoni hapo kujipatia mahitaji yake hali iliyopelekea wananchi kumfuata nyuma nyuma wakiamiani kuwa ndiye Rais hvy ametembelea sokoni hapo kwa kushitukiza.
Hata hvy mzee huyo baada ya kuona anafuatwa na kushangiliwa na watu aliamua kusimama ambapo alizungukwa na watu.Hatimaye alijieleza na watu wakamuelewa.Hata hvy watu wanafanana sn lkn hutofautiana kwa mengi.
Wanachi tunapaswa kuwa makini.

CHADEMA YASHINDA KESI.

Hatimaye mashauli yaliyokuwa yamefunguliwa mahakamani na waluokuwa wagombea Ubunge kupinga ushindi wa majimbo 2 mkoani Morogoro uliokwenda CHADEMA.Walalamikaji hao ambao waligombea kupitia CCM ktk majimbo ya Mlimba na Kilombero walifungua kesi hizo kupinga ushindi ambao Chadema ilishinda ktk majimbo hayo mawili ktk uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015.Mashauli yote ya kesi hizo yametupiliwa mbali na kwamba CHADEMA ilishinda kihalali.Huku Mh.Lijuwalikali aliyeshinda Kilombero na yule mwenzie wa Mlimba wakaahidi kwenda sasa kuwatumikia wananchi wao baada ya kuisha kwa kesi hizo.


MCHANA NA KATUNI.

Mpya kabisa,kuelekea Dodoma baada ya kutangazwa Serikali yote kuhamia huko,Taasisi,mashirika na wizara zote macho yao yote yameelekezwa huko.
Enjoy.

VIRAINISHI VYA MASHOGA VYAKAMATWA SHINYANGA.

Hatimaye mafuta ya KY JELLY yanayosadikiwa kutumiwa na Wanaume wanaojuhusisha na mapenzi ya jinsia moja(Mashoga)kama virainishi yakamatwa mtaa wa Kambarage mkoani Shinyanga.Virainishi hvy ambavyo hutumiwa kupaka njia ya haja kubwa wakati wa tendo vimekamatwa kupitia msako mkali ulioendeshwa na wizara ya afya wakishirikiana na jeshi la polisi.





Alhamisi, 28 Julai 2016

KWA HELI NEY WA MITEGO

Hatimaye baraza la Sanaa Tanzania(BASATA)Lamfungia kwa muda usiojulikana Msanii wa Hip Hop,Bwn.Ney wa Mitego.Balaza hilo limemtaka msanii huyo kutojihusisha na muziki tena hapa Nchini hadi hapo watakapoamua kumfungulia.
Wadau na mashabiki wa msanii huyo na Hip Hop kwa ujumla wamesema kwamba kufungiwa na kukatazwa kujihusisha na musiki halafu tena kwa muda usiyojulikana ni sawa na kumpoteza kavisa Ney wa Mitego ktk tasnia ya muziki nchini Tanzania.Msanii huyo aliyewahi kutamba na ngoma kibao na za ukweli ikiwemo "AM TRUE BOY" amekumbwa na kadhis hiyo baada ya kutoa ngoma yake mpya iitwayo "PALE KATI PATAMU"ambapo mashairi na video yake sito rafiki kwa maadili ya taifa hili.

WAZO LA LEO.


MAGAZETINI LEO

Pata nakala yako.

BURIANI JOSEPH SENGA.

Mwandishi wa Habari ambaye ndiye aliyepiga picha ktk kifo cha aliyekuwa Mwandishi wa Habari Daud Mwangosi mkoani Iringa 02/09/2012 ndugu Joseph Senga afariki Dunia.
Joseph amefariki Dunia jana SAA moja jioni nchini India alikokuwa akitibiwa.

Jumatano, 27 Julai 2016

UKAWA WAJA KIVINGINE

Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA ktk duru za kisiasa hapa nchini jana vimeanzisha umoja mwingine uitwao UKUTA.
UKUTA ni Umoja wa kupambana na Udikteta Tanzania.Umoja huo wenye lengo mahsusi la kuupinga ukandamizaji na demokrasia nchini umeanzishwa siku ya jana.Inadaiwa kuwa umoja huo ndiyo chachu ya ukombozi wa demokrasia ya kweli hapa nchini.





CHADEMA YAKANUSHA KIFO CHA NDESAMBURO

Chama cha Demokrasia na Maendeleo nchini CHADEMA kimekanusha uvumi wa taarifa zinazozidi kuenea mitandaoni kwamba Mbunge msaafu wa jimbo la Moshi mjini na M/kiti wa chama hicho Mkoani Kilimanjaro Mh.Ndesamburo kuwa ameaga Dunia usiku wa kuamkia leo kuwa Habari hizo ni za uongo.
Kupitia chanzo chetu cha Habari hii,ni kwamba Mh.Ndesamburo ni mzima kabisa wa afya akiendelea na shughuli zake za kila siku.Akizungumza kwa kujiamini ndugu Basili Lema amesema taarifa hzo potofu si za kutiliwa maanani kwani zinalenga kuupotosha umma na hasa wanachama wa chama hicho kuendelea na mambo ya msingi badala yake waanze kukimbizana na tukio hilo lisilo na ukweli.Hata hivyo amelaani vikali kwa wote wale wanaoendelea kuueneza uongo huo na kudai kuwa ni watu wabaya wasiyoitakia mema CHADEMA na hvy hawafai Hata kutazamwa usoni.

WAZO LA LEO.

Sasa kuanzia Leo furahia burudani nyingine tutakayokuwa tunakuletea iitwayo
WAZO LA LEO.Hapa tutapeana mielekeo chanya kuhusu maisha tu na si vingenevyo.
ENJOY.

MHUSIKA KIFO CHA MWANGOSI AHUKUMIWA.

Hatimaye ile kesi ya kifo cha aliyekuwa mwandishi wa habari mkoani Iringa nduku Daudi Mwangosi iliyokuwa ikimkabiri ndugu Pasificus Saimon yamalizika kwa mahakama kuu kanda ya Iringa kutoa hukumu hii leo.
Mshitakiwa huyo ambaye alikuwa ni askari wa jeshi la polisi kitengo cha kutuliza ghasia FFU Mjini Iringa amekutwa hatiani kwa kosa LA kuua bila kukusudia kitendo alichokitekeleza mnamo tarehe 02/09/2012 mkoani humor wakati mwandishi huyo akiwa kazini huku jeshi la polisi likiwajibika kuutawanya mkutano wa kisiasa wa CHADEMA wakati mikutano hiyo ikiwa imesitishwa kupisha zoezi la sensa ya watu na makazi iliyokuwa ikiendelea nchi nzima.
Mahakama hiyo imemuadhibu mshitakiwa Hugo kwenda jela miaka 15.



HATIMAYE BI CLINTON APITISHWA URAIS MAREKANI.

Hatimaye mwanasiasa wa kike nchini Marekani Bi.Hillary Clinton hii leo ameteuliwa na kutangazwa rasmi na chama chake cha Democrats(Democratic National Convetion)kuwa mgombea urais wa Marekani kupitia chama hicho.
Mwana mama huyo shupavu na mwenye sera zenye mvuto kwa Wamarekani wengi ktk hafla au mkutano huo mkuu uliohudhuriwa na wananchi,wanaharakati na wanasiasa mbalimbali alimuarika pia kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo kutoka Tanzania Mh.Zitto Zubery Kabwe.
Pamoja na hayo wananchi wa taifa hilo kubwa Duniani akiwemo Mumewe Bwana Clinton wameinesha kuwa na tumaini naye na kudai kwamba anafaa kuliongoza taifa hilo.





MAGAZETINI LEO.

Usikose nakala yako kupitia magazeti ya Leo 27/07/201


MAGEZETINI LEO.



Hakikisha unajipatia nakala yako Leo.Magazeti yetu ya Leo haya hapa

KOFF OLOMIDE JELA MWAKA NA NUSU CONGO.

Mwanamuziki nguli wa muziki wa dansi nchini Congo Koff Olomide Jana amehukumiwa kifungo cha kwenda jela miezi 18 ambayo in sawa na mwaka 1 na miezi 6.Mwanamuziki huyo alikumbwa na kadhia hiyo baada ya kuntwanga makofi mnenguwaji wake wa like ktk onesho.