Jumapili, 18 Septemba 2016

YANGA NA SIMBA ZANG'ARA VPL JANA,SERENGETI BOYS VS CONGO BURE LEO.

Jana ligi kuu soka Tanzania bara iliendelea viwanja mbalimbali nchini huku ikishuhudiwa mechi mbalimbli zikipigwa ambapo:
(1)Simba vs Azam~Uwanja wa Uhuru Dar.
(2)Mtibwa vs Kagera Sugar~Manungu Moro.
(3)Mbao FC vs Ruvu shooting~Mabatini
(4)Ndanda FC vs Majimaji~Mtwara
(5)Yanga vs Mwadui FC~CCM Jamhuri Kambarage.
(6)Prison vs Mbeya city~Sokoine Mbeya.
Kwa matokeo kiufupi ni kwamba pambano la Simba na Azamu,Simba ilitoka kidedea kwa kuirambisha Azam fursana moja bila majibu.
Huku mechi ya Yanga na Mwadui wakitoka 2 bila ktk dimba la CCM Jamhuri Kambarage kule Shinyanga mjini.Hata hivyo ktk pambano hilo zilitaka kupigwa ngumi kati ya makocha wa timu hizo  wakati wa mapumziko.Kocha wa Mwadui Julio na Pluigm wa Yanga waliamuliwa na ugomvi ukaishia hapo lkn chanzo cha zogo hilo bado hakikujulikana haraka zaidi inasemekana walirushiana maneno tu.
Kwa matokeo hayo Simba wanakaa kileleni mwa ligi hiyo kwa kuwa na point 13 huku Yanga ikipaa hadi nafasi ya pili mbele ya Azamu wao wakiwa nafasi ya tatu wote wakiwa na pointi 10 lkn wakitofautiana magoli ya kufunga na kufungwa ambapo Azam wao wameruhusu kufungwa magoli zaidi na kufungwa mechi moja na tayari wamecheza mechi zao 5 wakati Ynga wao wamecheza mechi 4 na hawafungwa hata moja huku wakishinda mechi 3 na mechi moja wakitoka suruhu ya bila kufungana.Pambano hill LA Yanga na Mwadui pia lilishuhudiwa NA na Waziri wa mambo ya ndani Mh.Mwigulu Lameck Nchemba.

Kwa hali nyingine isiyo ya kawaida hii leo kutakuwa na pambano zidi ya Serengeti boys ya Tanzania na Congo vijana chini ya miaka 17,huku mechi hiyo ya kuwania kushiriki kombe la mataifa Afrika kwa vijana wa umri wao likishuhudiwa bure kabisa yaani bila kiingilio zaidi ya miguu yako tu.
Hii imeelezwa jana na waziri mwenye dhamana ya michezo nchini Mh.Nape Nnauye.





















Hakuna maoni: