Jumatatu, 19 Septemba 2016

MZAZI WAKO NDIYE SHUJAA WAKO.

Pamoja na kwamba wapo waliotelekezwa ama kukataliwa na baadhi ya wazazi wao,lkn bado ukweli huu unabaki palepale ya kwamba rafiki wa kweli ni baba na mama au mmoja kati yao.Wengine wanaweza wakakutimizia mahitaji flani maisjani mwako ukahisi wanakupenda lkn tunda la roho lipo kwa mzazi aliyekuzaa.
Mtu baki atakusaidia kitu ili apate kitu,lkn mzazi wako kukusaidia kwake ni wajibu.
Mtu baki unaweza mkosea ukamwomba msamaha lkn akabaki na kinyongo juu yako lkn mzazi ana msamaha wa kweli.
Mtu baki anawezakuwa rafiki mtaka maslahi kwako,ama kukupenda kwa sababu ya kitu fulani ulichonacho,lkn mzazi yupo kukupa usichokuwanacho.
Mtu baki hata akifa leo mbele yako maumivu yake ktk kumpoteza si kama itakavyokuwa pindi unapompoteza mzazi.
Mtu baki atakusema vibaya vijiweni au hata kazini kwako kutokana na madhaifu yako,lkn mzazi huyatumia madhaifu yako kukufanya uwe bora.
Mzazi ndiye mwenye kukuwazia mema na mtu wa pili ktk kukufanikisha huku Mungu akiwa mtangulizi wake ktk hii Dunia.Haijalishi mzazi wako yukoje,mheshimu,mpe nafasi ya kuzijua na kukusaodia kuzitatua changamoto zako...,mzazi wako ndiye msiri wako kuliko hata huyo mpenzi wako.
Mtu baki anaweza achana na wewe akawa na mwingine lkn mama au baba hata iweje wanabakia kuwa hivyo tu..Kila ulalapo ama uamkapo mwombe Mungu awalinde wazazi wako ikiwa kama bado wako hai,lkn kama walishafariki waombee kwa Mungu awarehemu.

Eee,Mungu tunakuomba uwalinde na kuwazidisha wazazi wetu wote waliopo hapa Duniani,lkn pia tunaomba na kwa wale ambao umekwisha kuwatanguliza mbele za haki,Bwana uwarehemu,uwasamehe dhambi zao na kuwapumzisha kwa Amani.
Baba tunakuomba sisi wanao utupe,ufahamu,hekima,nidhamu na maarifa ktk kuyatumiza mapenzi yako juu yao hawa wazazi wetu tukitambua ya kuwa wewe ndiye uliwapa kibali kwamba kupitia wao sisi tukazaliwe.Tunaomba baba utukumbushe kuwaheshimu na kuwajali kwa hali na mali,lkn pia utusamehe sisi watoto ambao kwa namna moja ama nyingine tuliwatenda dhambi wazazi wetu iwe kwa maneno,kwa vitendo au hata kwa kutokuwatii.
Tunaomba yote hayo tukiamini na kuyapokea toka kwako,Amen.


Hakuna maoni: