Hatimaye pambano la soka la Kimataifa kwa umri chini ya miaka 17 limemalizika jioni hii jijini Dar es Salaam likiwakutanisha vijana wa Tanzania Serengeti Boys dhidi ya vijana wa Congo,ambapo timu ya taifa ya vijana chini ya umri miaka 17 Serengeti Boys yaichapa Congo magoli 3 kwa 2.
Mchezo huo ulokuwa wa kukata na shoka Serengeti Boys ndiyo walikuwa wa kwanza kutupia goli 2 bila majibu hadi kipindi cha kwanza kinakwisha,lkn kipindi cha pili cha mchezo Congo wakapata penati iliyowazalia goli 1,lkn dakika chache baadaye Serengeti Boys wakaongeza goli la 3 lilofungwa kiufundi mno na dakika ya 90 ya mchezo Congo wakionekana kufufuka wakaongeza goli la pili.
Hivyo kuufanya mchezo huo ukimalizika kwa Serengeti kushinda kwa bao hizo 3 dhidi ya 2 za Congo ambapo Serengeti boys walikuwa nyumbani.Mchezo mwingine wa marudiano utapigwa tena kule Congo bapo kama Serengeti Boys watashinda basi watakuwa ktk njia nzuri ya kufuzu kuingia kwenye makundi.
Lkn itakumbukwa kuwa jana Waziri mwenye dhamana ya michezo aliwaahidi kumpoza kila mchezaji Taslim Tsh.200,000/= na huku akiahidi kuwapa motisha ya Laki tano kwa kila goli litakalofungwa na vijana hao wa Serengeti Boys.
Sisi mnyausiblog.blogspot.com tunasema Ahsanteni Serengeti Boys kwa kutubeba Watanzania ktk michuano hiyo lkn pia pongezi na shukrani ziende kwa benchi lote la ufundi,TFF,pamoja naye Waziri Nape Nnauye kwa kulisapoti soka letu na michezo yoote kwa ujumla,lkn pia heko kwenu Watanzania wenzetu mliohudhuria na kuishangilia timu yetu.Ama hakika tutafika Inshaallah.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni