Binafsi naamini,na ninakueleza kuwa piga uwa,baba au mama yako ndiye shuja wako.Hata vitabu vya dini vilinena kwamba ni mzazi gani ambaye mwanaye akiomba mkate akampa jiwe???,jibu hakuna.
Hivyo mzazi wako ndiye mwenye kheri na laana maishani mwako.Yeye ndiye Mungu wako wa pili hapa Duniani.
Hebu jionee hapa.Huyu mtoto moto ulizuka nyumbani kwao,lkn mzazi badala ya kujiokoa yeye kwanza bado alianza na kumuokoa mwanaye kwa kumtoa ndani ya nyumba kupitia dirishani huku moto ukiendelea kushika kasi nyumbani humo.
Waheshimu wazazi wako kwa kadiri ya uweza wako,nakwambia Utayaishi maisha yenye kheri na baraka Duniani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni