Timu ya Taifa ya soka wanawake Kilimanjaro Qeens ya nchini Tanzania yatinga fainali za mabingwa Afrika kwa soka la wanawake baada ya kuisambaratisha Uganda Qeens kwa mabao 4 kwa 1 hiyo jana kule nchini Uganda.
Wakati Uganda wakikutana na aibu hiyo wakiwa nyumbani,huku kwetu nako vijana umri chini ya miaka 17 wa timu ya taifa ya Congo walionja ndimu baada ya vijana wa Tanzania Serengeti Boys kuwalambisha goli 3 kwa 2 pale jijini Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni