Ijumaa, 9 Septemba 2016

JAMES SIANG'A AAGA DUNIA.

Kocha aliyewahi kutamba na kikosi cha timu ya Simba nchini na nje ya nchi James Siang'a afariki Dunia.Siang'a amekutwa na umauti alfajiri ya kuamkia leo.
Siang'a anaondoka huku tungali bado tupo kwenye majonzi ya kumpoteza mchazi na kocha mwingine wa zamani wa timu za Pan Africa,Yanga na timu ya taifa Taifa Stars Mohamed Msomalia aliyetutoka juzi na jana kuzikwa mkoani kwao mjini Morogoro.
Mungu alitoa na Mungu ametwaa,jina lake lihimidiwe Daima.
KWA KHERI SIANG'A,hakika tutakukumbuka sisi wapenzi wa soka na Watanzania wote kwa ujumla.

Hakuna maoni: