Ulevi wa aina yoyote siyo mzuri kabisa kwa afya,taaluma,kiuchumi,kijamii hata kimaisha.
Utumiaji wa pombe kali hasa viroba umekithiri mno kwa vijana,mtu kutwa nzima analewa tu hali inayopelekea kuthoofu kiafya na zaidi tunapoteza tu nguvu kazi ya taifa.Uvutaji bangi na utumiaji ugoro navyo vimeshika kasi matokeo yake hata tunayoyafanya wakati mwingine ni vioja kama siyo aibu tu kwetu vijana na jamii kwa ujumla.
Mbali upigwaji vita juu ya uzalishaji,usambazaji na utumiaji wa vitu hivyo lkn bado tu utadhani ni sikio la kufa lisilosikia dawa.Bangi siyo nzuri,hebu muone huyu kavuta mwishowe anaogelea kwenye beseni akidhani yuko kwny swiming pool,huyu naye kipiga viroba hata hajielewi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni