Na Joachim Mkwawa.
Katika maisha ya kila Siku ya mwanadamu kitu mafanikio ni jambo muhimu sana kwake.Lakini vipi na kwa namna gani atafanikiwa ndivyo vitu ambavyo hufanya wengi washindwe kufanikiwa.
Leo nimekuletea
FUNGUO 10 ZA HEKIMA NA MAFANIKIO.
(1)MIPANGO
>Mafanikio yako hutegemea sana ubora wa mipango yako ya maandalizi.
>Moja ya sababu za kutokufanikiwa no kutokuwa tayari kutenga muda kwa ajili ya kupanga malengo thabiti.
>Mipango huleta kujiamini,kujali,kuheshimi na kukupa Ari ya kuitimiliza.
>Kitu cha muhimu katika ndoto zako ni kuwa na Mpango makini pamoja na Mpango kazi unaotekelezeka.
>Mipango huondoa migongano isiyo ya lazima.
(2)UTULIVU WA AKILI.
>Mbegu ya Mafanikio huota,hukua na kumea vema palipo na Amani.
>Usifanye chochote kinachousumbua moyo na kuitesa roho na nafsi yako.
>Gundua kile kinachokutia hamasa na kuamsha hisia na fikra zako katika maisha ili kufanikiwa.
>Mile kinachokupa Amani moyoni ndicho muhimu sana hasa kwa maisha yako.
>Chochote kiletacho furaha,Amani na nguvu ndani yako;ni alama ya kile Mungu anachotaka ufanye.
>Fanya kile unachokiamini na kukipenda kwani ndicho hukutafsiri.
>Itii dhamiri yako,ni ufunguo wako wa Mafanikio.
(3)NDOTO YAKO,MLENGO WAKO.
>Ndoto yako huhitaji sana mlengo wako wote.
>Mlengo wako utakufanya use MTU wa shauku,mbunifu na mvumilivu.
>Maisha ni safari hivyo yakupasa uwe na muelekeo.
>Ndoto yako huanzisha na kuchochea nia iliyo moyoni mwako.
>Mambo makubwa kwa kawaida huanza na mambo madogo.Mti mkubwa huanza na mbegu Ndogo.
>Watu Kushindwa kufanikiwa kwa sababu ya kuwa na muelekeo mbovu.
>Maisha yako ya kesho(baadaye)huanza na kile ulichonacho Leo mkononi mwako.
(4)MAUMIVU/MACHUNGU
>Kila aliyefanikiwa aligundua kuwa maumivu ni ya muda.Yatapita,ni njia ya kuelekea Mafanikio.
>Mtu hazami kwa kuangukia tu kwenye maji,Bali huzama endapo ataendelea tu kubaki ndani ya maji.
>Usiharibu ndoto,mipango,malengo na maisha yako ya baadaye kwa kufikiria tu maumivu yako ya nyuma.
>Huwezi zuia misiba isitokee,Bali unaweza kuikwepa isikuharibu wewe.
>Watu wakuu wamepitia maumivu makubwa.Mateso yako ni njia ya kuelekea miujiza yako mikubwa.
Jifunze kuvumilia na kuwa tayari kuzikabili changamoto ili kuifikia hatima yako maishani.
(5)UPENDELEO
>Usidharau wema unaotendewa na Watu.Siyo kitu kidogo katika Dunia hii kubwa.Ni kitu kikubwa sana katika Dunia hii ndogo.
>Wape wengine nafasi ya kwanza ili kupanda mbegu ya kupendelewa na kufanikiwa ama kufanikishwa katika maisha.
(6)HARAKA HARAKA
>Ndoto kubwa huhitaji muda zaidi.
>Unapoharakisha;Unaongeza makosa katika mambo yako.
>Fanya mambo kwa usahihi tokea mwanzo.
>Tumia vena muda wako ili kufanya mambo yako kwa usahihi.
>Mafanikio katika maisha hayaji kama ajali.
>Mafanikio ya maisha humgharimu MTU.
Hivyo lazima utambuwe kuwa itakugharimu wewe kufikia ukuu.Itakugharimu muda,nguvu,msimamo,kujitoa,kujituma,kujinyima na kuvumilia.
(7)MUDA
>Anayetumia muda wake vizuri hutawala maisha yake.
>Usipoteze muda.Ni mfupi sana,wenye thamani na haupatikani tena.
>Usiiache Siku ipite hivi hivi tu.
>Epuka kupoteza muda wako na marafiki,maongezi yasiyo na tija wala manufaa kwako.
>Watu wakuu huzitumia siku zao vizuri.
>Wasiyoheshimu muda wako,hawata heshimu HEKIMA yako.
>Muda ni pesa.
(8)KUSHINDWA
>Kushindwa hakuwezi kukutokea pasipo ruhusa yako.
>Kila binadamu hufanya makosa.
>Ushindi huenda kwa yule asiyekata tamaa.
>Kila Mtu hushindwa.Lakini wanaoshindwa huanza upya baada ya Kushindwa.
>Washindi huwa hawakubali Kushindwa.
>Vita ni vya wale waliyo wavumilivu.
>Maisha siyo mwendelezo wa Kushindwa;Bali huwa ni gwaride La miujiza.
>Acha kushughulikia mambo ya Jana.
>Mungu huwa haangalii yaliyopita ili kuamua hatima ya maisha yako ya baadaye.
>Kushindwa kwako huandaliwa na kuzimu Lakini Mafanikio yako huandaliwa na Mbingu.
(9)URAFIKI NA USHIRIKIANO
>Wasiyokuongezea kitu,Hukupunguzia kitu.
>Siyo Kila wanachokiongea Watu juu yako ndiyo muhimu.Ila kile unachokiamini wewe juu yako ndiyo muhimu.
>Washindi huwa hawafanikiwi peke yao.Bali hukishinda kiburi chao.Hukataa kuwa wapweke.
>Kila Mtu ni kisima cha taarifa.Chota kutoka kwake.
>Unachowafanyia Watu; Mungu hufanya kitokee kwako pia.
>Sifa zako nzuri zitaonekana mbele ya watu wazuri.
>Lipa gharama ili ukae miongoni mwa watu wa kawaida ili ufanikiwe.
>Usiongee matatizo yako na MTU ambaye hataweza kukusaidia kuyatatua.
>Marafiki hutofautiana;chagua wale wanaokuchangamsha,wanaokuelimisha na kukupa faraja.
>Hatua ya kwanza kuelekea kwenye Mafanikio ni kuwa tayari kusikiliza.
>Tumia HEKIMA ya watu wakuu ili ufanikiwe.
>Tumia vizuri nguvu au Mafanikio ya wengine.
>Mwongozo au ustawi ni ufunguo wa kufanikiwa.
(10)MABADILIKO
>Huwezi kuyabadilisha maisha yako hadi ubadili Yale uliyozoea kuyafanya kila Siku.
>Wakati mwingine hukulazimu ufanye kile usichokipenda ili upate kile unachohitaji na kukithamini.
>Huwezi kuinuliwa hadi utoke kwenye nafasi uliyopo sasa.
>Huwezi kusahihisha kile ambacho hauko tayari kuchukua hatua ya kukabiliana nacho.
>Hali ya maisha yako hutegemea sana mtazamo wako.
>Huwezi kufika unakokuhitaji kama hujaamua kunyanyua mguu kutoka hapo ulipo na kupiga hatua kwenda kule unakokutaka uwe.
>Huwezi kufikia malengo yako mpaka uyape kipaumbele katika mambo yako.
>Matatizo hutokea pale panapotokea mabadiliko.
>Kadiri unavyoendelea kukaa na tatizo ndivyo utakavyoshindwa kupata ufumbuzi.
>Leo ni kesho inayoongea kuhusu Jana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni