Alhamisi, 12 Machi 2020

UTENGENEZAJI WA CREAM YA KUNYOLEA.

Na Joachim Mkwawa.
Yes,
Leo tena nakualika darasani mtafutaji mwenzangu,Mjasiriamali na mwanamaono mwenzangu uliye na uchu wa kuwa mzalishaji na mmiliki wa kiwanda ama biashara yako na kuwaajiri wengine.
Karibu tujifunze KUTENGENEZA CREAM YA KUNYOLEA.
CREAM hii ni maalum kwa ajili ya KUNYOLEA NYWELE sehemu mbalimbali za mwili bila kukusababishia vipele ama muwasho wa aina yoyote ile na inakuacha msafi,mkavu na mwenye amani hadi zitakapoota NYWELE zingine.Ndiyo...

MAHITAJI/MALIGHAFI:-
(1)Asali.
(2)Castile.
(3)Mafuta ya vitamin E.
(4)Majani mabichi ya Mlimao,Mchungwa,Mkaratusi na Lavenda.
(5)Maji.
(6)Bees Wax.

JINSI YA KUTENGENEZA.
(1)Pima Bees wax robo kg weka kwenye sufuria.
(2)Twanga majani mabichi ya Mchungwa,Mlimao,Mkaratusi halafu kamua Maji yake;na upime vijiko 3 vya chakula kisha tia kwenye sufuria yenye Bees wax.
(3)Pima Asali vijiko 2 tia kwenye hiyo sufuria.
(4)Chukua Castile kijiko 1 cha chakula tia kwenye sufuria.
(5)Tia mafuta ya vitamin E vijiko 2 vya chakula kwenye sufuria.
(6)Chukua Lavenda vijiko 2 vya chakula tia humo kwenye sufuria.
(7)Chukua Maji vijiko 3 pia vya chakula tia kwenye hiyo hiyo sufuria.
~Baada ya kuchanganya pamoja kisha tenga sufuria yako Motoni.Acha mchanganyiko uchemke kiasi huku umeufunikia.
~Kisha ipua mchanganyiko huo Acha upoe huku ukiwa umeufunikia.

Baada ya hapo ukiona tayari mchanganyiko umeshapoa;umimine kwenye tube(tyubu/vifungashio)uliyoiandaa ili kuihifadhi CREAM yako tayari kwa matumizi ya kupaka sehemu uliyonyoa au tayari kwa biashara.

MUHIMU:-
Hakikisha moto uwe mdogo sana pindi unaichemsha cream yako.

Hii ni cream mmoja nzuri sana na ukiipatia utauza sana maana inapendwa kuliko spirit.
KUMBUKA tu kwamba MALIGHAFI zote tajwa hapo juu zipo na zinapatikana tu kwenye maduka maalumu ya Wajasiriamali nchi nzima.Na kuhusu majani yanapatikana sana kwenye mazingira yetu ya kawaida majumbani.

Ahsante sana.
Ni Mimi;
Joachim Mkwawa
Email:joachimmkwawa8@gmail
Simu:+255 625887699
          +255 710590088

Hakuna maoni: