Alhamisi, 12 Machi 2020

JE UNATAKA KUJUWA KUTENGENEZA SHAMPOO YA KUNG'ARISHA NYWELE?

Na Joachim Mkwawa.
Nichukue fursa hii kukukaribisha ewe mjasiriamali kwenye jukwaa hili pendwa kabisa La UJASIRI NI MALI(JIAJIRI).Mahala ambapo wajasiriamali na wazalishaji mbalimbali hujengwa na kuandaliwa kumiliki viwanda vyao binafsi vidogo vidogo.
Mada yetu Leo nataka UJUWE KUTENGENEZA SHAMPOO YA KUNG'ARISHIA NYWELE.
KUMBUKA:-
Hapa nakufunza kwa nadhalia lakini ukitaka kujifunza kwa vitendo Andaa muda wako na ada kidogo tu kisha nitafute ujifunze.Karibu darasani muda huu.

MALIGHAFI/MAHITAJI:-
(1)CDE
(2)Castile Soap
(3)Asali
(4)Distilled water
(5)Rangi
(6)Perfume.

JINSI YA KUTENGENEZA
(1)CDE nusu lita.
(2)Asali vijiko 3 vya chakula.
(3)Castile Soap robo kg.
(4)Distilled water robo lita.
(5)Rangi kijiko 1 cha chakula.
(6)Perfume vijiko 2 vya chakula.
(7)Changanya vitu vyote hivyo pamoja kama ulivyopima kwenye chombo kimoja.Koroga mchanganyiko huo kuelekea upande mmoja;hadi uhakikishe umechanganyika vizuri.

Na hadi hapo shampoo yako itakuwa tayari kwa matumizi.Ukitaka kuiuza basi nakushauri kwamba tafuta vifungashio tia humor shampoo yako,tia au bandika nembo yako tayari kwa biashara.Huhitaji kuweka chumvi.

Ahsante.
By
Joachim Mkwawa
Email:joachimmkwawa8@gmail.com
Simu:+255 625887699
          +255 710590088

Hakuna maoni: