Jumatano, 18 Machi 2020

CORONA;WENGINE WAWILI WAGUNDULIKA NA KUTANGAZWA.

Nchini Tanzania ugonjwa wa Corona wawakumba watu wengine wawili;mmoja akiwa ni Raia wa Marekani aliyegundulika jijini Dar es Salaam na mgonjwa wa pili ni Raia wa Ujerumani ambapo yeye amegundulika akiwa visiwani Zanzibar.
Maambukizi hayo mapya yanafanya kufikia kwa idadi ya watu watatu ambao ndiyo waliyothibitishwa na kuripotiwa na Wizara ya Afya ya Tanzania kupitia Waziri wa wizara hiyo Mheshimiwa Ummi Mwalimu.

Wagonjwa hao watatu ni pamoja na yule mwanamama wa miaka 46 aliyeripotiwa juzi tarehe 16/03/2020 jijini Arusha ambaye ni Raia wa Tanzania akitokea nchini Ubelgiji.
Aidha Mheshimiwa Ummi Mwalimu amesisitiza kuwa Serikali imejiandaa vema kuhakikisha inapambana na Corona na kwamba kila mwananchi anapaswa kuchukua tahadhari kubwa kuhakikisha anajilinda dhidi ya maambukizi ya ugonjwa huu hatari.
Chanzo:Channel10

Hakuna maoni: