Jumatano, 25 Machi 2020

TANGAZO:-NAFASI ZA KAZI.

Wanahitajika
(1)Mfamasia-Kuuza duka la dawa
(2)Mhudumu/Wakala-Huduma za kifedha(Tigopesa,M.pesa,Halopesa,Airtel money)


Vigezo:-
Mfamasia
~Cheti cha Nursing assistant
~Cheti cha Ado
~Cheti cha Form 4
~Umri kuanzia miaka 18-35
~Awe Mtanzania na aliye tayari kufanya Kazi bila kusimamiwa.

Mhudumu/Wakala
~Barua toka serikali ya Mtaa anakotoka.
~Uzoefu wa masuala ya mitandao ya simu.
~Awe Mtanzania na mkazi wa Dodoma.
Piga simu +255 653890025 au +255 626176465
NB:-
Usibip wala kutuma SMS hautajibiwa.

TANGAZO:NAFAZI ZA KAZI WIZARA YA AFYA

TANGAZO LA nafasi za kazi upande Udaktari.TANGAZO LA Wizara ya Afya.



Jumamosi, 21 Machi 2020

UMEME:-TANZANIA YAONGOZA AFRIKA KWA VIJIJI VYENYE UMEME.

Wizara ya Nishati nchini yathibitisha hilo.

Q.CHILA AFUNGUKA KUHUSU FA KUKUMBWA NA CORONA.

Msanii mkongwe wa Muziki wa Bongo fleva nchini Tanzania;Q Chila amesema kwamba kuhusu msanii mwenzake wa Muziki huo nchini Mwana FA kupatwa na Maambukizi ya Virusi vya CORONA inawezekana isiwe kweli Bali ni kiki tu.
Hutu hapa msanii Q'Chief ukipenda Q'Chila akifunguka.

Ijumaa, 20 Machi 2020

KUPIGWA TUNAJITAKIA

Hello team
Nimerejea na segment yetu ile toka kitambo.Hapa ndipo huwa tunanyoosha palipopinda.Ni makavu live tu.Haijalishi itakuuma kiasi gani.
Ujuwe mara nyingi KUPIGWA huwa hakuji tu hivihivi.KUPIGWA siyo lazima kweli MTU akushike na kuanza kukupiga kama wengineo mnavyofikiria;laa hasha.
Wakati mwingine kuibiwa Mali yako ni KUPIGWA,Kurogwa ni kupigwa pia.

Kujitakia ni pale ambapo Mtu unafahamu fika kwamba kufanyaje jambo Fulani hata kama halikukatazwa ni vibaya ama si kitendo cha kiungwana lakini cha ajabu kwa makusudi tu MTU anaamua kufanyaje buku unajuwa ni kosa kufanya hivyo.
Sasa mfano wewe mdada Mtu mzima na akili zako tens usikute unaishi na wazazi wako hasa mzazi wako wa kiume unaishi naye nyumba moja na Halafu bila woga kweli unapofua nguo zako za ndani na kuzianika nje tena umezisambaza kamba nzima ni sawa??.
Hebu fikiria mfano mdogo wako wa kiume aliyebarehe anaka mlangoni au kibarazani macho kayatumbulia kwenye kamba anaona kufuli(chupi)zako zilivuozagaa inakuwaje??.Kwa hiyo anjuwa kumbe Dada ana kufuli rangi hii,na ile na ile jamani.Sasa mfano ndo umeanika tu baba yako anaingia anakuta upepo umezidonsha kufuli mbichi kadhaa hapo chini.Atakuita we Fulani njoo nguo zimedondoka,au atainama aziokote na kuzitundika tena kambani ama???.Wengineo mpo kwenye nyumba za kupanga uswahilini huko Halafu unaanika mikufuli yako hovyo hovyo ndiyo nini??.Wadada wengi siku hizi wanahangaika na uzazi lakini ukiwachunguza kwa vipimo mahospitali unakuta wako vizuri lakini mimba hawapati na hawajui ni kwa nini.Moja ya sababu ni uanikaji hovyo wa nguo zao za ndani.Hapo umeanika mfano Mtu mbaya akaifanyia mazingara hujadhurika??.Ama watoto wakishaona hadharani hujiheshimu na minguo unaanika hovyo watakuheshimu kweli??.
Aaaah peleka huko.Wakati mwingine KUPIGWA MNAJITAKIA.
Joachim Mkwawa
mnyausiblog.blogspot.com

MUZIKI;WASAFI(WCB)WAANZISHA BENDI.

Lebo ya Muziki ya Wasafi chini ya CEO wake Diamond Platinums imeamua kukusanya wasanii mbalimbali na kuanzisha bendi.Uamuzi huo umekuja baada ya kuusoma vema mchezo na mwenendo ama muelekeo wa muziki ulivyo hivi sasa ndani na nje ya nchi.
Kundi hill La wasanii(bendi)linasemekana linaundwa na idadi kubwa ya wasanii waliyokuwa wakiunda kundi La Yamoto Band kipindi cha chuma.

Kwa mujibu wa chanzo chetu ni kwamba Wasanii kutoka Yamoto Band na ambao wanatarajiwa kuwa sehemu ya bendi hiyo mpya toka Wasafi(WCB)ni pamoja na Enock Bella,Mboso,Bella na wengineo buku msanii Lava Lava akitajwa kuwa kiongozi wa kundi hilo ndani ya bendi yao hiyo mpya.Huku msanii Aslay akikosekana ndani take.
Mnyausi News tutaendelea kukujuza hatua kwa hatua juu ya hili.

RELATIONSHIPS:-

THE REASONS WHY YOUR RELATIONSHIPS DON'T LAST.
Joachim Mkwawa.

Many Relationships these days take a drastic turn after few months.
Most time it's not intended,or planed by the partners but it becomes unavoidable so as to save the friendship that once existed.
These nosedive does not just happen it may be as a repetition of some characters or attitudes which one or both spouse detest.

Relationships are like newborns and must be handled as such else it will not survive.Your Relationships don't last because of these reasons listed below;

(1)You do not take each other into considerations before making vital decisions;
√As little as this may seem it has a way of making the other person feel insignificant or useless;the next thing on their mind will be how to exist the relationship.
It may even start building inferiority complex in them.Making them feel they are valueless and no one wants to stay where they are irrelevant.

(2)You did not take out time to check out your comparability;
√Many a times people jump into a relationship immediately they fell small butterflies in their stomach, not realizing that with time those will fly away as they came and they will be left with regality to face.
Whether we like it or not,the truth is we can not be comparable with everyone no matter how much we like them initially. True colors will start unfolding with time.

(3)You do not Realize that they have a mind of their own;
√Yes,most times we get blinded with love that we forget to remember that we are still dealing with Humans that have their sense intact and hence should have a mind of their own.So,most times when making decisions we should left them give their input, argue with ours and not.

(4)You are not open to change;
√Some of us have grown so rigid with time that we do not realize how important change is to is and the world of large.
When you a letting someone into your heart and space of large;You must take place with time because of individual differences. You should be ready to adjust some things to accommodate the other.
Relationships are all about little comprises from time to time.
By;
Joachim Mkwawa
Motivational Speaker
New Vision with Common Skills.
mnyausiblog.blogspot.com

If you find this to be true;please feel free to drop comments and share the article.

Jumatano, 18 Machi 2020

CORONA;WENGINE WAWILI WAGUNDULIKA NA KUTANGAZWA.

Nchini Tanzania ugonjwa wa Corona wawakumba watu wengine wawili;mmoja akiwa ni Raia wa Marekani aliyegundulika jijini Dar es Salaam na mgonjwa wa pili ni Raia wa Ujerumani ambapo yeye amegundulika akiwa visiwani Zanzibar.
Maambukizi hayo mapya yanafanya kufikia kwa idadi ya watu watatu ambao ndiyo waliyothibitishwa na kuripotiwa na Wizara ya Afya ya Tanzania kupitia Waziri wa wizara hiyo Mheshimiwa Ummi Mwalimu.

Wagonjwa hao watatu ni pamoja na yule mwanamama wa miaka 46 aliyeripotiwa juzi tarehe 16/03/2020 jijini Arusha ambaye ni Raia wa Tanzania akitokea nchini Ubelgiji.
Aidha Mheshimiwa Ummi Mwalimu amesisitiza kuwa Serikali imejiandaa vema kuhakikisha inapambana na Corona na kwamba kila mwananchi anapaswa kuchukua tahadhari kubwa kuhakikisha anajilinda dhidi ya maambukizi ya ugonjwa huu hatari.
Chanzo:Channel10

Jumatatu, 16 Machi 2020

CORONA YABISHA HODI TANZANIA.WAZIRI WA AFYA ATHIBITISHA.

Mapema asubuhi ya Leo Machi 16 Wizara ya Afya kupitia Waziri wake Mheshimiwa Ummi Mwalimu(MB)imesema kwamba mgonjwa hiyo ni mwanamke(46)Aligundulika kuwa na maambukizi ya virus 19 vya ugonjwa wa Corona.
Ikiwa hiki ndicho kisa cha kwanza cha ugonjwa huo kugundulika ambapo mwanamke huyo alisafiri akitokea nchini Ubelgiji kuja nchini Tanzania na kushuka Uwanja wa ndege wa Kilimanjaro(KIA).
Chanzo:Milad Ayo(Ayo TV)

Jumamosi, 14 Machi 2020

PRAYERS NEEDED HERE.

Joachim Mkwawa.

Please we're inviting you to pray with Gloria.
My name is Gloria;
I see how people pray for sick people on social media's. I have 3 kids and my husband is late.
Please pray for me as I want to do this surgery.I know some people will ignore me but remember you can be in my condition tomorrow.
I don't want to die;help me by praying and sharing this post to others.Am at the point of death.Please share it as much.

EDUCATION IS POWERFUL.

Education is more powerful in life.
That why we send our children to school to get education.
Education is tool which can be used for exploring the Universes and Lives of the Creatures.

Mnyausi News;
We're agreed that every child should go to school.
Yet in our Countries especially in our rural areas,Children are still burdened with early Marriage, engaged at farming and never feel even their Childhood time.
And those are exerctly the kind of reasons;That's make us Mnyausi News to start this campaign.
Every Child deserves a Childhood and it's up the rest of us to help remove the Barrie's that stand in their way.
"Please make it easier for all the masses".
Joachim Mkwawa
Motivational Speaker.

Ijumaa, 13 Machi 2020

IJUWE VIZURI CORONA NA JINSI YA KUJIKINGA NAYO.

Na Joachim Mkwawa.

Kila kona Duniani hivi sasa lugha inayoongewa ni moja tu.Nayo si nyingine ni juu ya kuenea kwa virusi vya ugonjwa wa ajabu na hatari wa Corona.
Corona unaripotiwa kuwa ni ugonjwa hatari sana ambao umekuwa tishio si tu kwa kukatisha uhai wa binadamu haraka Bali hata kudumaza ama kuwa tishio kwa uchumi wa Mataifa mbalimbali Duniani.Kwa Sasa kesi nyingi za Ugonjwa huu zinaripotiwa karibia Mabara yote Duniani na hasa kwa mataifa makubwa kama China,Italia,na kwingineko watu wakizidi kuambukizana na hata kupoteza maisha kwa wingi.
Basi kwa kuzingatia hayo Mnyausi News tumekuletea video yenye elimu juu ya ugonjwa huu hatari na namna ya kujikinga nao.

RAIS MAGUFULI ATOA TAHADHARI KUHUSU CORONA

Na Joachim Mkwawa.
Hii leo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Pombe Magufuli atoa onyo Kali kwa wananchi wake wote wa Tanzania juu ya ugonjwa hatari na tishio kwa uchumi wa Dunia;ugonjwa wa Corona.
Asisitiza kwamba Corona ni ugonjwa hatari na unaogharimu(kuua)maisha ya binadamu hataka kuliko magonjwa mengine.
Rais Magufuli akiongea hayo ameonya pia juu ya Tabia za watu wanaopenda kusafiri hovyo ndani na nje ya nchi.Kila Mtu katika familia yake nchini Tanzania anao wajibu wa kuchukua hatua kujilinda na kuelemisha wengine juu ya janga hili La Dunia.
Mtizame mheshimiwa Rais John Magufuli kupitia video hii.

ACHA MOYO WAKO UONGEE.

Habari za wakati huu ndugu mpendwa na msomaji wetu wa blog hii pendwa.
Nachukua fursa hii adhim kukueleza ya kwamba haijalishi ni yepi magumu unayapitia wakati kutokana na sababu mbalimbali za kimaisha.Naomba nikwambie kwamba yote unayoyapitia ni sehemu tu ya mchakato wa kukufanya ama kukutengeneza kuwa bora kulingana na hatima yako maishani.
USILIE.ACHA MOYO WAKO UONGEE.

Alhamisi, 12 Machi 2020

UTENGENEZAJI WA CREAM YA KUNYOLEA.

Na Joachim Mkwawa.
Yes,
Leo tena nakualika darasani mtafutaji mwenzangu,Mjasiriamali na mwanamaono mwenzangu uliye na uchu wa kuwa mzalishaji na mmiliki wa kiwanda ama biashara yako na kuwaajiri wengine.
Karibu tujifunze KUTENGENEZA CREAM YA KUNYOLEA.
CREAM hii ni maalum kwa ajili ya KUNYOLEA NYWELE sehemu mbalimbali za mwili bila kukusababishia vipele ama muwasho wa aina yoyote ile na inakuacha msafi,mkavu na mwenye amani hadi zitakapoota NYWELE zingine.Ndiyo...

MAHITAJI/MALIGHAFI:-
(1)Asali.
(2)Castile.
(3)Mafuta ya vitamin E.
(4)Majani mabichi ya Mlimao,Mchungwa,Mkaratusi na Lavenda.
(5)Maji.
(6)Bees Wax.

JINSI YA KUTENGENEZA.
(1)Pima Bees wax robo kg weka kwenye sufuria.
(2)Twanga majani mabichi ya Mchungwa,Mlimao,Mkaratusi halafu kamua Maji yake;na upime vijiko 3 vya chakula kisha tia kwenye sufuria yenye Bees wax.
(3)Pima Asali vijiko 2 tia kwenye hiyo sufuria.
(4)Chukua Castile kijiko 1 cha chakula tia kwenye sufuria.
(5)Tia mafuta ya vitamin E vijiko 2 vya chakula kwenye sufuria.
(6)Chukua Lavenda vijiko 2 vya chakula tia humo kwenye sufuria.
(7)Chukua Maji vijiko 3 pia vya chakula tia kwenye hiyo hiyo sufuria.
~Baada ya kuchanganya pamoja kisha tenga sufuria yako Motoni.Acha mchanganyiko uchemke kiasi huku umeufunikia.
~Kisha ipua mchanganyiko huo Acha upoe huku ukiwa umeufunikia.

Baada ya hapo ukiona tayari mchanganyiko umeshapoa;umimine kwenye tube(tyubu/vifungashio)uliyoiandaa ili kuihifadhi CREAM yako tayari kwa matumizi ya kupaka sehemu uliyonyoa au tayari kwa biashara.

MUHIMU:-
Hakikisha moto uwe mdogo sana pindi unaichemsha cream yako.

Hii ni cream mmoja nzuri sana na ukiipatia utauza sana maana inapendwa kuliko spirit.
KUMBUKA tu kwamba MALIGHAFI zote tajwa hapo juu zipo na zinapatikana tu kwenye maduka maalumu ya Wajasiriamali nchi nzima.Na kuhusu majani yanapatikana sana kwenye mazingira yetu ya kawaida majumbani.

Ahsante sana.
Ni Mimi;
Joachim Mkwawa
Email:joachimmkwawa8@gmail
Simu:+255 625887699
          +255 710590088

JE UNATAKA KUJUWA KUTENGENEZA SHAMPOO YA KUNG'ARISHA NYWELE?

Na Joachim Mkwawa.
Nichukue fursa hii kukukaribisha ewe mjasiriamali kwenye jukwaa hili pendwa kabisa La UJASIRI NI MALI(JIAJIRI).Mahala ambapo wajasiriamali na wazalishaji mbalimbali hujengwa na kuandaliwa kumiliki viwanda vyao binafsi vidogo vidogo.
Mada yetu Leo nataka UJUWE KUTENGENEZA SHAMPOO YA KUNG'ARISHIA NYWELE.
KUMBUKA:-
Hapa nakufunza kwa nadhalia lakini ukitaka kujifunza kwa vitendo Andaa muda wako na ada kidogo tu kisha nitafute ujifunze.Karibu darasani muda huu.

MALIGHAFI/MAHITAJI:-
(1)CDE
(2)Castile Soap
(3)Asali
(4)Distilled water
(5)Rangi
(6)Perfume.

JINSI YA KUTENGENEZA
(1)CDE nusu lita.
(2)Asali vijiko 3 vya chakula.
(3)Castile Soap robo kg.
(4)Distilled water robo lita.
(5)Rangi kijiko 1 cha chakula.
(6)Perfume vijiko 2 vya chakula.
(7)Changanya vitu vyote hivyo pamoja kama ulivyopima kwenye chombo kimoja.Koroga mchanganyiko huo kuelekea upande mmoja;hadi uhakikishe umechanganyika vizuri.

Na hadi hapo shampoo yako itakuwa tayari kwa matumizi.Ukitaka kuiuza basi nakushauri kwamba tafuta vifungashio tia humor shampoo yako,tia au bandika nembo yako tayari kwa biashara.Huhitaji kuweka chumvi.

Ahsante.
By
Joachim Mkwawa
Email:joachimmkwawa8@gmail.com
Simu:+255 625887699
          +255 710590088

JIFUNZE KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI.

Na Joachim Mkwawa.
Karibu tena ndugu msomaji na mjasiriamali mwenzangu katika dawati hili La UJASIRI NI MALI(JIAJIRI)ili uchote maarifa.
Na Leo nataka ujifunze KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI.

Sabuni hii ya MAJI unaweza itumia kudekia ndani kwako(nyumbani),kufulia au kama utataka kuitumia kwa ajili ya kusafishia maliwatoni(choo na bafu)Basi huna budi kuongeza kiwango cha perfume kidogo wakati wa kuitengeneza.
Hebu ungana nami hapa chini hatua kwa hatua ujuwe.

MAHITAJI/MALIGHAFI:-
(1)Salfoniki asidi nusu lita.
(2)Slees robo kg
(3)Sodash robo kg
(4)Maji lita 15
(5)Rangi nusu kijiko
(6)Sodiamu salfeti nusu kg
(7)Perfume vijiko 2
(8)Formaline vijiko 2
(9)Glyceline vijiko 4.

JINSI YA KUTENGENEZA.
(1)Andaa Diaba(jana)au chombo chochote cha ujazo wa lita 20.
(2)Weka Maji kiasi kwenye chombo chako.Hakikisha chombo chako ni kikubwa na kina ujazo unaozidi wingi wa Maji yako.
(3)Weka Salfoniki Asidi,Slees koroga kisha weka Maji tena na uendelee kukoroga kuelekea upande mmoja.Yaani unakoroga kuelekea kulia usigeuze kuelekea kushoto.
(4)Weka Sodash,Rangi uipendayo,Perfume, Formaline na Glyceline kisha endelea kukoroga mchanganyiko huo kwa dakika 2 au 3.
(5)Chukua chombo kingine cha plastiki mfano jagi au bakuli,chota huo mchanganyiko wako kiasi kupitia jagi au bakuli kisha chukua sodiamu tia kwenye hill jaki au bakuli lenye mchanganyiko uliyouchota toka kwenye jaba;halafu koroga ili sodiamu ichanganyike vizuri.Baada ya hapo mimina huo mchanganyiko wa kwenye bakuli au jagi umiminie kwenye ule mchanganyiko mwingi wa awali uliyomo kwenye jaba na uendelee tu kukoroga ndani ya jaba huku unaumimina mkorogo uliyomo kwenye bakuli au jagi.

Na hapo utaanza kuona mkorogo/mchanganyiko wako unaanza kupanda(kuongezeka/kuumuka)kuja juu.Kwa nini inakuwa hivyo??.
Ni kwa sababu Sodiamu huongeza wingi wa sabuni yako.Hivyo ukikoroga lita 15 hakikisha chombo chako kiwe kina ujazo wa lita 20 au zaidi.

Formaline husaidia kuitunza sabuni yako isiharibike haraka;yaani ukiweka Formaline basi sabuni yako inaweza kaa hata mwaka 1 bila kuharibika.
Ukimaliza,weka sabuni yako kwenye vifungashio(parkeg) tayari kwa biashara na matumizi.

KUMBUKA:-
Kuna aina 5 za Formaline.
(1)Formaline ya Chakula.
(2)Formaline ya Dawa.
(3)Formaline ya Sabuni.
(4)Formaline ya Maiti.
(5)Formaline ya kuzuia wadudu wasiharibu lotion.
Hivyo kuwa makini sana wakati wa kununua Formaline kulingana na uhitaji wako ama unakwenda kuitumia kufanyia nini.

MALIGHAFI zote hizo zipo na zinapatikana kwenye maduka maalum ya wajasiriamali nchi nzima.
Ukizingatia na kufuata vema hatua hizo hapo juu utakuwa hodari sana na mzalishaji mkubwa wa sabuni hii ya Maji.
Ahsante.
Wako ktk ujenzi wa Taifa
Joachim Mkwawa
Email:-joachimmkwawa8@gmail.com
Call/WhatsApp +255 625887699.

NAMNA YA KUTENGEBEZA SABUNI YA MCHE.

Na Joachim L.Mkwawa

Sabuni ya mche unawezaitumia kufulia,kuogea ama kuoshea vyombo nk.
Namna ya kutengeneza sabuni ya mche.

MALIGHAFI:-
(1)Mafuta ya Mbosa/mawese/Nazi Lita 4.
(2)Maji mililita 350×4=1400;ambazo ni sawa chupa 4 za soda zilizojaa vizuri.
(3)Caustic Soda 0.5kg
(4)Sodash 0.5 kikombe cha chai.
(5)Perfume.
(6)Box.

JINSI YA KUTENGENEZA:
Zingatia hatua zifuatazo pamoja na vipimo kama ninavyoelekeza ili utengeneze kitu bora,salama na chenye uhakika sokoni.
(1)Loweka Caustic Soda 0.5kg kwenye maji mililita 1400.
~Koroga na uifunike.Uache mkorogo huo ulale Massa 24 had I kesho.
(2)Kesho yake pasha moto mafuta.
~Ipua acha yapoe ibakie joto kiasi.
~Kisha yamimine mafuta hayo kwenye chombo kingine cha plastiki.
(3)Chukua Caustic Soda uliyoikoroga jana imimine kidogo kidogo kwenye chombo kile cha plastiki ulichoweka mafuta; huku ukikoroga haraka haraka kuelekea upande mmoja.
(4)Baada ya hapo koroga Sodash kwenye chombo kingine,kisha imimine kwenye mchanganyiko wa Caustic Soda na Mafuta huku ukiendelea kukoroga kuelekea upande mmoja.
(5)Weka perfume vijiko 2 vya chakula kisha koroga hadi uji uji use raini kabisa.
(6)Andaa box;mimina mkorogo huo ndani ya box.Acha ilale humor hadi kesho yake.
(7)Baada ya hapo utakata vipande vipande uvitakavyo wewe na Sabuni yako ya mche itakuwa tayari kwa matumizi.

Kwa maelezo zaidi ama kujifunza kwa vitendo tafadhali wasiliana nami kupitia +255 625887699 au +255 710590088.