Jumapili, 18 Desemba 2016

KUPIGWA TUNAJITAKIA.

Habari ndugu msomaji wetu,Tunatumai umzima wa afya.
Wakati mwingine ni wazi kabisa kwamba kupigwa tunajitakia sisi wenyewe.Na kupigwa siyo kupata majeraha tu bali hata kushitakiwa mahakamani kutokana na vitendo viovu tunavyovitenda tena wakati mwingine kwa makusudi kabisa huku tukijuwa kwamba tuyatendayo ni kinyume cha sheria na haki za binadamu.
Sasa hebu tizama mtu kama huyu kitendo anachokifanya kwa mke na mtoto wake.Je,mtu kama huyu kwanza amelewa halafu kwa hili analolifanya akiwajibiahwa utasema kaonewa????

Aaaah,tupigwe tu.Maana tunajitakia.

Jumapili, 11 Desemba 2016

MCHANA NA KATUNI

Habari gari ndugu msomaji wetu,Tunaomba radhi kwa kutokukuhabarisha kwa muda mrefu....,hii ilitokana na sababu ambazo hazikuwa chini ya uwezo wetu.

Hebu leo furahi nasi kwa katuni hii.

Jumatano, 26 Oktoba 2016

YANGA YAIKANYA VEMA JKT RUVU LEO

Hatimaye mchezo wa soka ligi kuu bara dhidi ya Yanga na JKT Ruvu uliochezwa Leo jioni umemalizika kwa time ya maafande wa JKT Ruvu kukubali kipigo cha jumla ya magoli 4 kwa 0.
Kwa ushindi huo bado Yanga inabaki nafasi ya pili kwa pointing 24 nyuma ya vinara wa ligi hiyo Simba SC yenye jumla ya pointing 29 ktk msimamo wa ligi hiyo ya Vodacom.Hats hivyo Yanga walionekana bado wako vizuri mbali na aliyekuwa kocha wao mkuu Hans Pruijym kujihudhuru kuifindisha time hiyo hivi juzi.

Jumapili, 23 Oktoba 2016

WAZO LA LEO


YANGA YATAKATA UWANJA WA KAITABA.

Mabingwa watetezi ligi kuu soka Tanzania bara time ya soka ya Yanga Jana ilitakata baada ya kuivunja vunja vibaya time ya soka ya Kagera Sugar ya mkoani Kagera ktk mechi ya ligi kuu vodacom Tanzania Bars.
Mchezo huo mgumu uliishuhudia Yanga ikiibuka na ushindi mnono wa magoli 6 kwa  2..

Kwa ushindi huo time hiyo ya Yanga yenye maskani take katikati ya mitaa ya Twigs na Jangwani jijini Dar es Salaam inakuwa nafasi ya pili ktk msimamo wa ligi hiyo ikiwa na jumla ya poiti 21 nyuma ya vinara wa ligi hiyo Simba sports Club yenye pointing 26 huku Stand United ya mjini Shinyanga ikiwa nafasi ya 3 kwa jumla ya ponti 21 pia lkn ikizidiwa na Yang's kwa zaidi ya mgoli.

Jumamosi, 22 Oktoba 2016

MCHANA WA VIOJA

Enjoy kioja hiki.

Alhamisi, 20 Oktoba 2016

UPENDO NI TIBA KWA NAFSI ILIYOJERUHIWA.

Tuwapende wenzenu kama vile sisi nasi tunataka tupendwe.Ubaguzi wa aina yoyote ile ni dhambi,kwani hujenga chuki na uvunjifu wa Amani miongoni mwetu,bila upendo hakuna ushirikiano na pasipo ushirikiano hakuna maendeleo.
NAKUPENDA NDUGU YANGU.

KUPIGWA TUNAJITAKIA.

Kupigwa huwa hakuji hivi hivi tu na kama ikitokea umepigwa bila sababu tunasema UMEONEWA lkn vinginevyo no makosa uloyafanya kwa makusudi huku unajuwa kuwa kwa kufanya hvy no makosa kisheria.

Jumapili, 2 Oktoba 2016

GOLI LA TAMBWE LAIGHARIMU SIMBA.

Ktk mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara kati ya Simba na Yanga ambayo ilichezwa jana na kushuhudia timu hizo hasimu zikitoka sare ya goli moja kwa moja huku goli la Amis Tambwe wa Yanga likisababisha mashabiki wa timu ya Simba waking'oa viti.Inasemekana kuwa zaidi ya viti 200 vilivunjwa na vingine kuharibiwa vibaya.
Kwa hali hiyo kuna hati hati ya Simba kupigwa faini,kuporwa pointi au hata kuamuriwa vyovyote vile itakavyoonekana inafaa lkn pia siyo dalili nzuri kwa ukuaji wa soka letu.

Jumamosi, 1 Oktoba 2016

KUPIGWA TUNAJITAKIA.

Ni pale ambapo MTU hufanya makosa ktk jambo Fulani.Hata ukikosea kuoa au kuolewa kupugwa.We unajijuwa kabisa kwamba huna nguvu halafu unaoa mwanamke mbabe unategemea nini.
MPIGWE TU,MAANA MNAJITAKIA.

SIMBA YACHOMOA KWA YANGA

Hatimaye pambano la soka kati ya Simba na Yanga jana lilimalizika kwa sare  ya bao moja kwa moja baada ya Simba kulazimisha mchezo uishe hivyo baada ya mchezaji wao Kichuya kusawazisha kupitia kona iliyotymbukia kimiani moja kwa moja.Yanga ndiyo walikuwa wa kwanza kuliona lango la wekundu hao wa Msimbazi kupitia kwa mchezaji wa kigeni Amisi Tambwe.
Hata hivyo mchezo huo uliingiwa na vurugu kwa mashabiki wa Simba kung'oa viti kwa kile kilichodaiwa ni hasira kutokana na goli la mkono lililofungwa na Tambwe wa Yanga na mwamuzi kuamuru mpira upigwe kati yaani ni goli.
Kwa sare hiyo bado inaifanya Simba iendelee kukaa kileleni mwa ligi ikiwa na pointing zake 17 ikiwa imekwisha cheza mechi 7 huku Yanga ikiwa nafasi ya pili kwa pointing 11 kibindoni huku ikiwa na mechi 6 ilizokwisha kucheza na kipolo cha mechi moja.

MCHANA NA KATUNI

Enjoy katuni zetu za Leo tukiangazia watani wa jadi ktk mechi yao ya Jana ligi kuu Vodacom Tanzania bara.
Shuhudia tambo zao hapa.

Alhamisi, 29 Septemba 2016

KILICHOJILI KTK KIKAO CHA KUMVUA UANACHAMA LIPUMBA.

Hizi hapa video za kikao cha CUF kilichomfua uanachama wa chama chama hicho Prof.Lipumba.

MAGAZETINI LEO

Yaliyojili kwenye magaze ya Leo 29/09/2016


Jumanne, 27 Septemba 2016

RAIS WA ZAMANI WA ISRAEL AFARIKI DUNIA.

Aliyewahi kuwa Waziri Mkuu na Raid wa zamani wa Israel Mh.Shimon Peres afariki Dunia mapema Leo hii.
Shimon alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kiharusi.Tayari Rais Obama wa Marekani mapema hii ametuma salamu za rambirambi kwa nchi ya Israel.

Jumatatu, 26 Septemba 2016

MCHANA NA KATUNI.

Kuelekea mechi ya Simba na Yanga jumamosi hii,tayari tambo na kebehi mbalimbali kwa watani hao wajadi zapamba moto.

Jumamosi, 24 Septemba 2016

MAGAZETINI LEO

Hizi hapa nakala za magazeti ya Leo 24/09/2015.


Alhamisi, 22 Septemba 2016

WAZO LA LEO


UPENDO NI TIBA KWA NAFSI ILIYOJERUHIWA

Penda ili upendwe.
Palipo na Upendo pana mafanikio,utajiri,amani,huruma,uvumilivu na kujali.
Pasipo upendo kuna machafuko.Tupendane jamani.




MCHANA NA KATUNI


MCHANA WA VIOJA


Jumatatu, 19 Septemba 2016

KUPIGWA TUNAJITAKIA.

Huyu mtu kwa lolote litakalomtokea ana wajibu wa kuyapokea.
(1)Anachafua mazingira
(2)Anachafua maji
(3)Anahatarisha afya za watumiaji wengine wa maji.
(4)Anajisaidia sehemu isiyostahili.
Aaaaah,tupigwe tu coz tunajikia.

MCHANA NA KATUNI


UTAMADUNI WETU.

Leo bado tumesalia hapahapa mkoani Dodoma tukiangazia ngoma za asili za wenyeji wa mkoa huu ambao ni Wagogo,Warangi na Wanyambwa.Lkn leo bado tuko na Wagogo ambao wao wamechukua sehemu kubwa sana ya mkoa huu hasa katikati,mashariki na kusini mwa mkoa huu wamejaa wagogo.Hebu leo wasikilize kikundi cha Nyota kutoka kabila hili la Wagogo kutoka wilayani Chamwino.
Unaweza tuandikia barua kupitia
 joachimmkwawa8@gmail.com
+255-629108340
+255-629114323.

TAMTHILIA:-TENDA WEMA NENDA ZAKO.

Karibu tens ewe mpendwa msomaji wetu upendezwaye na blog hii adhimu ya mnyausiblog.blogspot.com
Leo tunakuletea tamthilia fupi na nzuri iitwayo TENDA WEMA NENDA ZAKO.
Karibu,
  Siku moja ktk kijiji fulani cha wavuvi kilichokuwa pembezoni mwa bahari,wavuvi waliingia baharini kuvua samaki,lkn wakiwa bahatini ghafla wakaona kitu kikielea.Je,waliona nini?Shuka nayo hapa chini>>>











WAZO LA LEO



MZAZI WAKO NDIYE SHUJAA WAKO.

Pamoja na kwamba wapo waliotelekezwa ama kukataliwa na baadhi ya wazazi wao,lkn bado ukweli huu unabaki palepale ya kwamba rafiki wa kweli ni baba na mama au mmoja kati yao.Wengine wanaweza wakakutimizia mahitaji flani maisjani mwako ukahisi wanakupenda lkn tunda la roho lipo kwa mzazi aliyekuzaa.
Mtu baki atakusaidia kitu ili apate kitu,lkn mzazi wako kukusaidia kwake ni wajibu.
Mtu baki unaweza mkosea ukamwomba msamaha lkn akabaki na kinyongo juu yako lkn mzazi ana msamaha wa kweli.
Mtu baki anawezakuwa rafiki mtaka maslahi kwako,ama kukupenda kwa sababu ya kitu fulani ulichonacho,lkn mzazi yupo kukupa usichokuwanacho.
Mtu baki hata akifa leo mbele yako maumivu yake ktk kumpoteza si kama itakavyokuwa pindi unapompoteza mzazi.
Mtu baki atakusema vibaya vijiweni au hata kazini kwako kutokana na madhaifu yako,lkn mzazi huyatumia madhaifu yako kukufanya uwe bora.
Mzazi ndiye mwenye kukuwazia mema na mtu wa pili ktk kukufanikisha huku Mungu akiwa mtangulizi wake ktk hii Dunia.Haijalishi mzazi wako yukoje,mheshimu,mpe nafasi ya kuzijua na kukusaodia kuzitatua changamoto zako...,mzazi wako ndiye msiri wako kuliko hata huyo mpenzi wako.
Mtu baki anaweza achana na wewe akawa na mwingine lkn mama au baba hata iweje wanabakia kuwa hivyo tu..Kila ulalapo ama uamkapo mwombe Mungu awalinde wazazi wako ikiwa kama bado wako hai,lkn kama walishafariki waombee kwa Mungu awarehemu.

Eee,Mungu tunakuomba uwalinde na kuwazidisha wazazi wetu wote waliopo hapa Duniani,lkn pia tunaomba na kwa wale ambao umekwisha kuwatanguliza mbele za haki,Bwana uwarehemu,uwasamehe dhambi zao na kuwapumzisha kwa Amani.
Baba tunakuomba sisi wanao utupe,ufahamu,hekima,nidhamu na maarifa ktk kuyatumiza mapenzi yako juu yao hawa wazazi wetu tukitambua ya kuwa wewe ndiye uliwapa kibali kwamba kupitia wao sisi tukazaliwe.Tunaomba baba utukumbushe kuwaheshimu na kuwajali kwa hali na mali,lkn pia utusamehe sisi watoto ambao kwa namna moja ama nyingine tuliwatenda dhambi wazazi wetu iwe kwa maneno,kwa vitendo au hata kwa kutokuwatii.
Tunaomba yote hayo tukiamini na kuyapokea toka kwako,Amen.