Hatimaye pambano la soka kati ya Simba na Yanga jana lilimalizika kwa sare ya bao moja kwa moja baada ya Simba kulazimisha mchezo uishe hivyo baada ya mchezaji wao Kichuya kusawazisha kupitia kona iliyotymbukia kimiani moja kwa moja.Yanga ndiyo walikuwa wa kwanza kuliona lango la wekundu hao wa Msimbazi kupitia kwa mchezaji wa kigeni Amisi Tambwe.
Hata hivyo mchezo huo uliingiwa na vurugu kwa mashabiki wa Simba kung'oa viti kwa kile kilichodaiwa ni hasira kutokana na goli la mkono lililofungwa na Tambwe wa Yanga na mwamuzi kuamuru mpira upigwe kati yaani ni goli.
Kwa sare hiyo bado inaifanya Simba iendelee kukaa kileleni mwa ligi ikiwa na pointing zake 17 ikiwa imekwisha cheza mechi 7 huku Yanga ikiwa nafasi ya pili kwa pointing 11 kibindoni huku ikiwa na mechi 6 ilizokwisha kucheza na kipolo cha mechi moja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni