Ijumaa, 24 Aprili 2020

MBUNGE DEVOTHA MINJA APAMBANA NA CORONA MOROGORO

Mbunge wa Vitu maalum Morogoro mjini kupitia CHADEMA Mh.Devotha Minja;hii Leo amesaidia Wananchi mbalimbali wa Kata 15 za Manispaa ya Morogoro kwa kuingia mitaani na kugawa Barakoa 5000 kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya COVID-19.
Barakoa hizo zimegawiwa kwa makundi mbalimbali wakiwemo walemavu,mama ntilie,bodaboda,madeleva na makondakta wa daladala,wasari na watu mbalimbali wakubwa kwa Wagogo lengo likiwa ni kuonesha kwa vitendo juhudi zake katika kuhakikisha Wananchi wanajikinga na kuwa salama dhidi ya Corona ugonjwa ambao umekuwa tishio kwa afya uhai wa binadamu.






JIFUNZE KUTENGENEZA BARAKOA(MASK),COVID-19 INAUA.

Habari mpendwa msomaji wetu wa blog hii pendwa.
Natumai umzima wa afya lakini hongera kwa mapambano dhidi ya CORONA maana hili ni janga kubwa linalotutesa Duniani kote.
Leo mjasiriamali mwenzangu naomba nikushirikishe na kukuhamasisha kuhusu fursa iliyopo kutoka na janga hili(COVID-19).
Fursa hii itakuwa ni msaada kwanza kwako wewe mwenyewe lkn pia kwa familia na jamii inayokuzunguka kwa ujumla.
Unaweza kuwekeza Tsh.30'000/=(Elfu thelathini) na lakini ikakufanya kuingiza kipato mara 2 hadi 3 ya pesa uliyoiwekeza kila siku.Fanya hivi ingia dukani nunua kitambaa na lactic kisha mptafute fundi mzuri wa kushona Mpe akutengenezee barakoa(mask)kisha ingia Nazi masokoni,stendi za mabasi,au hata majumbani na uziuze kwa bei rafiki kwa mteja.Hapo utasidia jamii kujikinga na CORONA lakini pia utapata kipato.
Lakini hapa nimekuwekea video ya namna/jinsi rahisi ya kutengeneza barakoa za aina mbalimbali.

NGOMA ASILI:WAGOGO KUTOKA DODOMA TANZANIA.

Leo tunakusogea ngoma ya Asili kutoka kwa Kabila La Wagogo lenye maskani yake jijini Dodoma.Kwa kawaida ngoma hii huchezwa wakati kiangazi baada ya mavuno.Yaani nyakati za mapumziko baada ya kipindi kirefu cha kilimo kumalizika.Lakini pia ngoma hii huchezwa wakati wa sherehe mbalimbali za kawaida,Kiserikali na kimila.
Karibu ufurahie.
Ngoma hii huitwa "Mheme".
Na hiki ni kikundi cha ngoma Asili kiitwacho Nyota kutoka kijijini Majeleko,wilaya ya Chamwino jijini Dodoma.
Mimi ni Joachim Mkwawa.

Jumatatu, 20 Aprili 2020

VISA 84 VIPYA VYA COVID-19 VYARIPOTIWA TANZANIA HII LEO.

Wizara ya Afya nchini Tanzania yatangaza visa vipya 84 vya Corona.Na hivyo kufanya kufikia visa 254 tangu kuripotiwa kwa mara ya kwanza kuwepo kwa maambukizi ya Corona nchini.
Wananchi wote wameendelea kukumbushwa kuchukua tahadhari kama inavyoshauriwa na Wataalam wa Afya ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huu hatari.Tahadhari hizo ni pamoja na kunawa mikono kwa maji safi na sabuni maalumu kila mara,kuvaa barakoa,kuepuka misongamano na mikusanyiko isiyo ya lazima nk.


VITUKO VYA CORONA:KAMANDA AKAGUA GWARIDE

Covid-19 imeleta vituko ambavyo ni darasa la kujifunza.Kila mmoja hivi sasa anajaribu kubuni njia sahihi atakayoitumia kuelimisha jamii inayomzunguka kuhusu janga la Corona linaloiendesha Dunia hivi sasa.Tizama video hii Kamanda akikagua GWARIDE la Corona.

MANENO YA MWISHO YA MCH.GEDTRUDE RWAKATARE

Haya ndiyo maneno yake ya mwisho marehemu Asikofu Mama Gertrude Rwakatare alipohubiri ibadani.Na hapa anazungumzia kuhusu Covid-19 sambamba na magonjwa mengine ya milipuko(Tauni) kama yalivyotabiriwa kwenye kitabu kitakatifu(Biblia).Mama Gertrude Rwakatare alikuwa Askofu wa kabisa la Mlima wa Moto la jijini Dar es Salaam.
Askofu Rwakatare amekutwa na umauti alfajiri ya leo akiwa Hospitali ya Mloganzila alipokuwa akipatiwa matibabu.Tutakukumbuka sana mama yetu hasa kwa huduma yako bila kusahau ule"UPEPO WA KISULISULI".
Mungu akulaze pahala pema,Amen.

VITUKO VYA CORONA:WAUMINI WARUSHIWA MEZA YA BWANA.

Corona imefanya tunashuhudia vituko vingi sana Duniani kote.
Hats hivyo vituko hivi vimekuwa msaada sana katika kuifunza jamii namna ya kujikinga ama kuepuka maambukizi mapya ya Covid-19.
Hebu tazama video hii.

Jumamosi, 18 Aprili 2020

MAFURIKO YASABABISHA MAAFA UVIRA NCHINI CONGO

Hali bado ni tete ama mbaya tarafa ya Uvira;huko nchini Congo.Baada ya miili ya watu kupatikana ikiwa imetapakaa mitaani.Hali hii imekuja baada ya maji yaliyotokana na mafuriko kuanza kupungua.
Miili ya watu zaidi ya 30 imeopolewa ikiwemo ya watoto wachanga.
Wakazi wa tarafa hii ya Uvira wameiomba serikali na Rais wa Congo kuwahi kupeleka misaada ya kibinadamu kabla ya magonjwa ya milipuko kuanza kutokea.
  Kutokana na jiografia na ukubwa wa nchi ya Congo pamoja na hali ya miundombinu ya eneo hilo bado Serikali haijafika Uvira kutoka Kinshasa.
Watu zaidi ya laki moja mjini Uvira hawana makazi wala Chakula.





MWANGA WA AJABU ULIVYOTOKEA NA KUSHANGAZA WATU KARIAKOO NCHINI TANZANIA

Juzi siku ya jumatano mitaa ya Kariakoo jijini Dar es Salaam nchini Tanzania kulitokea hali ya ajabu na ya kushangaza ambapo kulitokea ishara za ajabu na kushangaza zilizotanda barabara kwenye anga La jiji hilo huku hali hiyo ikiwaacha watu katika mshangao wa aina yake.
Wadau na watu mbalimbali kwa imani zao walitolea ufafanuzi/utabiri juu ya halo hiyo.

Ijumaa, 17 Aprili 2020

KENYA:-WADAU WALALAMIKIA UNYANYASWAJI WA WATU WEUSI NCHINI CHINA.

Watu,wadau na Viongozi mbalimbali kutoka ukanda wa Afrika ya Mashariki wameendekea kulamikia na kulaani vikali juu ya vitendo visivyo vya kibinadamu wanavyofanyiwa Waafrika nchini China.
Ungana nami kwenye hii video.

HATUA 6 MUHIMU KATIKA MAISHA YA MWANADAMU

KUTOKA IBADANI.
Habari ndugu msomaji na mfuatiliaji wetu wa blog hii pendwa.
Tunatumai umzima wa afya.Awali ya yote tunatoa salamu za pole kwa wagonjwa wote wa COVID-19 Ulimwenguni kote,Pia pole kwa viongozi na wafiwa wote Duniani kutokana visa na vifo vitokanavyo na janga hili la Corona.Hata hivyo tunachukua fursa hii kuwakumbusha watu wote kuchukua hatua na tahadhali mbalimbali katika kujikinga na maambukizi ya ugonjwa juu hatari.Aidha tunawakumbusha kila mmoja wetu kuchukua hatua ya kuelimisha wengine kuhusu COVID-19 na namna ya kujikinga na zaidi sana tunashauri tubaki majumbani tukiwa salama.
   Mpya hii Leo ni kwamba kuanzia Leo Mnyausiblog tutaanza kukuletea makala za mafundisho Kutoka Ibadani kupitia watumishi mbalimbali wa Mungu wanaohudumu makanisani na misikitini.
Lengo la safi hii ni kukuelimisha na kukuburudisha zaidi na zaidi.
Ni furaha na wajibu kwetu kukuona unaelimika na kukua kiungu(kiimani)na maisha kiujumla.
Leo tunaye Mchungaji Peter Mitimingi kutoka Tanzania akiwa na somo la
HATUA 6 MUHIMU ANAZOZIPITIA MWANADAMU KATIKA MAISHA.
Karibu ujifunze.

Alhamisi, 9 Aprili 2020

SONGA MBELE USIRUDI NYUMA.

Yeah!!;
Ya mkini kuna mambo unayapitia ni magumu sana kwako,unaona ni mtihani mkubwa sana kwako kuufauru.Ama yawezekana uko na maumivu makali sana yanayoutesa moyo wako.Umefukuzwa kazi,unatafuta kazi hupati,umetengwa,umefeli mitihani,unaugua ama unauguza.Umepoteza wapendwa wako,tumaini la maisha hulioni na unahisi kunyanyasika sana moyoni mwako na mengineyo kama hayo;Basi ndugu yangu ninakusihi kwamba usife moyo kwa sababu changamoto kamwe huwa hazikimbiwi.Changamoto zipo ili kutufanya tujijenge na kwa bora zaidi Kule tuendako.
Kamwe huwezi toka darasa moja kwenda kingine ikiwa hukuufauru mtihani.Unayoyapitia Leo ni mtihani tu.Usikate tamaa,nyanyuka usonge MBELE.Simama uendelee na safari;ushindi wako upo.SONGA MBELE USIKATE TAMAA.
Joachim Mkwawa
Motivational Sleeker
mnyausiblog.blogspot.com

Jumanne, 7 Aprili 2020

KUPIGWA TUNAJITAKIA

Leo sina maneno mengi sana kueleza.Lakini kifuatacho kinajieleza wazi kabisa ya kwamba mambo mengine huwa tunajitakia.
Ndiyo!;Kupigwa Tunajitakia.
Joachim Mkwawa.
mnyausiblog.blogspot.com

Jumamosi, 4 Aprili 2020

JINSI YA KUANZISHA BIASHARA

Joachim Mkwawa & Noa Ubongo.

Hello
Team wachapakazi,wapambanaji,wachakalikaji na wazee wote wa mihanjo mjini.
Natumai site tuko poa kabisa.
Najuwa kila mmoja wetu yuko na ndoto za kumiliki biashara yake mwenyewe si ndiyo??.
Basi kama kawaida yangu Mnyausi nipo hapa kukusogezea nondo mbalimbali za kukuvusha pindi unaiendea hatima yako maishani.Hii ni Mnyausiblog na chombo kwa hewa hivi sasa ni UJASIRI NI MALI(JIAJIRI),huku mada mezani ikisomeka kama:-

JINSI YA KUANZISHA BIASHARA.
Vipo vingi vya muhimu kujifunza na kuvijuwa kabla ya kuanzisha biashara.
Yamkini waweza kuwa tayari ulikwisha wahi kujaribu kuanzisha biashara ikafa ama bado inaendelea nk;lakini leo nimekusogezea maarifa zaidi yatakayo kuongezea fahamu na kufanikiwa kibiashara.Darasa hili pia unalipata YouTube channel yetu jina Joachim Mkwawa,hakikisha una subscribe na ubonyeze kengere nyekundu ili uwe wa kwanza kupata videos mbalimbali za mafunzo tunazoziweka humor.
Mimi ni;
Joachim Leonard Mkwawa
Motivational Speaker
mnyausiblog.blogspot.com

Ijumaa, 3 Aprili 2020

TIME TO RETHINK ABOUT LIFE.

With
Mr.Criss

Emptiness and Vanity!.
Our cars are just parked there,no where to go to.The private jets are lying in waste,air spaces are all shut,every country nursing its Citizens and fighting an unseentiny enemy.
Each man is confined to a room in those big mansions and the designer;clothes,bags,shoes,perfumes and make-up kits have all become useless and serving no purpose.
No more urgent appointments and business meetings that diprive us of time with our Creator and family.
No parties to attend and hangouts to meet up with friends,no more canvoys and sirens,even the money stocked away in the accounts and slack always are useless....

Even our expansive and expensive church auditoriums are empty,it is now each man with his Creator in truth and air to breathe,we just want to be alive.Nothing else is really important.
This World has never seen vanity as it is today!.

Good News is;we all have one more chance to introspect,to reflect and ask,"Why does my Creator need to keep me alive through this?,To marry or buy new cars or perhaps finish my doctorate or receive my blessings from professed men of God?".
What is my purpose in life now and after COVID-19?.
Why does my Creator need to spare me and allow others die?.
Of what value am I to humanity and to my Creator and His Kingdom that should make Him to spare me?.
Let us pray and change our ways and seek a more purposeful living after COVID-19.
May God help us to seek Him the more.
This too shall pass.
Joachim Leonard Mkwawa
Motivational Speaker
mnyausiblog.blogspot.com

Alhamisi, 2 Aprili 2020

JINSI YA KUBAKI KUWA MASIKINI(THREAD)

Na Joachim Mkwawa
Motivational Speaker.

Habari mwanadawati mwenzangu wa dawati hill la UJASIRI NI MALI(JIAJIRI).
Dawati ambalo kimsingi hukujenga na kukuhamasisha katika kujiajiri wewe mwenyewe ama kuwekeza hata kama upo katika ajira rasmi.
Dawati hill kipekee ndilo hupatikana na kutukutanisha wajasiriamali kupitia blog hii pendwa Duniani kote.Na Leo nimewiwa kukushirikisha hatua ama mambo muhimu ya kuzingatia ikiwa unataka KUBAKI KUWA MASIKINI MAISHANI MWAKO.

JINSI YA KUBAKI KUWA MASIKINI.
Yamkini unaweza usinielewe;lakini kufuatia hatua hizi naamini ukizifuata na kuzifanyia kazi kikamilifu hakika lazima ubaki kwenye umasiki.
(1)Kamwe usiamke mapema,Endelea kulala na kujinyoosha.We lala tu hadi jua litakapochomoza,yaan hakikisha unalala hadi uone mwanga wa ndani kwako unafana na wa nje.Au lala hadi njaa itakapokuuma ndipo uamke.
(2)Kamwe usipange namna sahihi ya kuitumia pesa yako.We zitumie tu utakavyo hasa pale unapozipata.Na zikiisha hata usipoteze muda kukaa chini na kufikiria ulizitumiaje.
(3)Kamwe usiwaze wala kufikiria ku-save pesa yako,subiri hadi upate pesa nyingi ndipo uanze ku-save.Uta-save vipi pesa yako wakati unazo kidogo!??.Tena wapuuze wale wote wanaokushauri ku-save kwani hawakutakii mema wewe na pesa yako.Watakupangiaje kutumia pesa yako ilihali hawakukusaidia kuitafuta??.
(4)Kamwe usijiingize kwenye biashara ambazo huwa mnaziita za kitoto tena ni za watu wasiyosoma.Wewe ni msomi bwana na tena umemaliza chuo kikuu,umeajiriwa na halafu unalipwa vizuri mshahara mkubwa.Sasa ya nini ufanye biashara za kuuza Viazi?,Utauzaje mbogamboga?,Yaani na usomi wako halafu ukauze viatu vya mtumba kweli?.We msomi bwana hupaswi kufanyaje biashara za watu wasiyosoma aisee.Wewe unafaa ukae tu ofisini upigwe na kiyoyozi Basi.Una shida gani kwani.
(5)Kamwe usifikirie kuanzisha biashara mpaka pale Malaika atakaposhuka kutoka Mbinguni akuletee mtaji mkubwa wa kuanzisha biashara.Kwa wakwambie uanzishe biashara hata kwa mtaji mdogo eti kisa wafanyabiashara wengine wakubwa kama akina MO au Bakhresa walianza kwa kuuza migahawa.Wewe ni smart bwana unatakiwa uanze na mamilioni.Sawa eeeh!??.
(6)We lalamika kuhusu kila kitu Ila Kamwe usilalamike kuhusu uvivu wako na Attitude yako.We ilaumu tu Serikali ya Magufuli kwamba imekaza vyuma,Lalamikia benki zisizotaka kukuamini na kukukopesha mtaji,laumu makampuni mbalimbali yaliyokunyima ajira ama yaliyokufuta kazi.Kwa sababu wote hao ni wabaya na hawataki wewe uwe tajiri.
(7)Tumia pesa nyingi kuliko kipato chako.Na ili kufanikisha hilo wewe tununua bidhaa kwa mkopo,azima pesa kwa rafiki zako,nunua samani nzuri za ndani,Nunua Brand New LG flat screen.Kopa pesa benki ama kazini kisha kanunue gari Kali na ya kisasa ya kutembelea.Honga vyovyote vile utakavyo hadi mjini wakukome.Ndiyo pesa si ni zako bwana;unakwama wapi?.
(8)Shindana katika kuvaa.Hakikisha hupitwi na fashion yoyote mpya ya nguo,viatu,gari na simu.Nunua kila aina ya simu inayotoka yaani usikubali kupitwa na Toledo jipya la simu;hata kama ulikuwa na Samsung Galaxy S6 uliyoinunua milioni 1 we iuze tu hata kwa laki 7 kisha ongezea pesa kiasi uende kununua Samsung Galaxy S7.Ndiyo kwa sababu hizo simu kalikali zimetengenezwa kwa ajili yako bwana.
(9)Ukishindwa kununua gari mpya,Nunua hata used lakini Kali na ambayo gharama zake kwenye kuihudumia ni mara 2 ya mshahara wako ama inayodumu muda mrefu.
(10)Halafu mwisho sawa wala usiogope maneno ya watu.Maana watu kama wewe msiyokuwa serious na maisha huwa hamzeeki wala nini.Endelea kuishi hivyo hivyo.
Fainali ni uzeeni.
Hivyo ajili za kuambiwa vema ukachanganya na za kwako.
Ukifanya kinyume na hizo hatua lazima utatajirika na ikiwa utazifuata na kuzitii vema hizo hatua Basi naamini umasikini utakuhusu.
Mimi ni
Joachim Leonard Mkwawa
Motivational Speaker
mnyausiblog.blogspot.com