Hii leo kunako dimba la Taifa kumeshuhudiwa mchezo wa nguvu ukiwakutanisha mabingwa watetezi Simba SC ya jijini Dar es Saalam dhidi ya Stand United ya Shinyanga.
Ambapo hadi dakika 90 za mchezo kumalizika Simba ilitoka kifua mbele kwa ushindi mnono wa magoli 3 kwa 0 huku magoli hayo yakitiwa kimiani na wachezaji Cletous Fhama mnamo dakika ya 30 wakati la pili likifungwa na Emmanuel Anord Okwi huku lile la 3 likiwa ni la kujifunga Stand Utd wenyewe baada ya kutokea harakati za uokoaji wa mpira wa kona ulipigwa na Shiza Ramadhan Kichuya mnamo dakika ya 86 ya mchezo.
Kwa ushindi huo ni kudhihirisha kwamba kile walixhokieleza wachezaji kabla mchezo huu hapo jana ni kwamba watashinda mechi hiyo ya kesho(leo)ili iwe ndiyo pole yao kwa Boss wao aliyekuwa kapotea kwa kutekwa kwa zaidi ya siku 8 kabla ya kupatikana usiku wa kuamkia jana.
Mbali na hivyo Simba watakuwa wameendelea kujiweka pazuri zaidi ktk msimamo wa ligi kuu Bara wakiwa na pointi zao 17 kwa michezo 8 nyuma ya mahasimu wao Yanga SC wanye pointi 19 kwa michezo 7 huku vinara ktk msimamo huo wakiwa ni Azam FC zote za jijini Dar es Saalam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni