Ijumaa, 19 Oktoba 2018

MANJI RASMI YANGA.

WANACHAMA NA MASHABIKI MENO NJE NJE.
Habari ndiyo hiyo unaambiwa.
Ni kwamba Mara baada ya kujiweka pembeni dhidi ya soka na hasa timu ya Yanga kwa zaidi ya siku 517 ambazo ni sawa na mwaka 1 na miezi 4 na siku 29...,hatimaye Tajiri,mfadhiri,mwenyekiti na kipenzi cha wana Yanga Bw.Yusuph Manji amerejea na kutambuliwa kama ndiye mwenyekiti wa klabu hiyo kongwe na mabingwa wa kihistoria kunako tasnia ya kandanda nchini Tanzania.

Yusuph Manji alitangaza kujiuzuru kuitumikia Yanga km Mwwnyekiti mnamo mwezi Mey tarehe 20 mwaka 2018.
Kutokuwepo ama kutojihusisha kwake dhidi ya Yanga kuliifanya timu hiyo kuyumba kiasi fulani kiuchumi,kiufundi na hata kushindwa kuutetea ubingwa wao waliyokuwa wakiushikilia kwa matatu mfurulizo hadi mwaka jana.
Mbali hayo timu ilishindwa hata kusafirisha wachezaji baadhi ilipitakiwa kucheza ugenini(mikoani) mfano wa ile mechi kati yao na timu mojawapo ya jijini Mbeya mwaka jana.

Hayo,ni matikeo ya kikao cha kamati ya uchaguzi ndani ya klabu hiyo kilichokaaliwa juzi jumatano  ambapo kilitoka na maazimio ya kumrejesha na kumtambua Manji kama ndiye Mwenyikiti wa timu hiyo huku kamati hiyo ikisisitiza kwamba nafasi zilizowazi na zinazotakiwa kupata viongozi ni Makamu mwenyekiti pamoja nafasi za wajumbe ambao waliyokuwepo awali walijihuzuru nyazifa zao wakiwemo;Salum Mkemi,Hashim Abdallah na Omar Saidi kutoka Tanzania Visiwani(Zanzibar),Huku Ayoub Nyenzi kwa kutohudhuria vikao mfururizo vya kamati hiyo hivyo naye alipoteza sifa za kuwa mjumbe wa kamati hiyo ya Utendaji ndani ya klabu.

Itakumbukwa pia nafasi ya makamu mwenyekiti ilikuwa chini ya Clement Sanga aliyejihuzuru nafasi hiyo.

Hata hivyo Katibu mkuu wa klabu hiyo Bw.Omary Kaya alieleza kwamba habari zote kuhusu Mwenyekiti alidai lipo chini ya kamati ya uchaguzi ambayo ndiyo yenye dhamana ya kulisemea hilo huku  mjumbe wa kamati ya uchaguzi wa Yanga,Bakili Makele alisema kuwa ufafanuzi wa zoezi la uchaguzi na kwamba ni lini utafanyika na habari zote za Manji utatolewa kwenye mkutano na vyombo vya habari muda wowote kuanzia leo Ijumaa.

Wakati hayo yakielezwa na viongozi hao huku wadau,wanachama na mashabiki kindakindaki wa timu hiyo kongwe nchini wameonekana wakifurahia urejeo huo wa bosi huyo kipenzi wa Yanga huku wakitamba kwamba taji la ubingwa ni lao na kwamba wao ndiyo wanastahili kukwea pipa(kupanda ndege)kwenda kuiwakilisha nchi ktk medani za kimataifa.

Hakuna maoni: