Jumanne, 28 Machi 2017

MCHANA NA KATUNI

Enjoy mchana wako kwa katuni kali toka kweti

MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO.

Samaki mkunje angali mbichi Wahenga walisema.Na mtoto umleavyo ndvy akuavyo.Wakati mwingine wazazi hujutia mambo yanayoweza kuwakumba hasa yanapotendwa na watoto wao.Malezi mabovu hukuza mtoto mwenye akili mbovu.

Jumamosi, 25 Machi 2017

GARI INAHITAJIKA.

Mwenye gari Langelover sport toleo la 2012 or Namba D na anataka kuiuza basi kuna mtu anaihitaji fasta.
Wasiliana na muhitaji kwa Namba 0717-139333 mfanye biashara.

Ijumaa, 24 Machi 2017

MZAZI WAKO NDIYE SHUJA WAKO

Habari yako mpedwa msomaji wetu,karibu tena ktk ukurasa wetu huu adhimu unaolenga kutukumbusha kama jamii hasa vijana Duniani kote kwamba tufanye vyote vile lkn mwisho wa siku tuwakumbuke wazazi ama walezi wetu ambao walituzaa na kutulea kwa hali na mali na kutufanya tufike hapa tulipo leo.Haijalishi unayopitia,umefanikiwa ama hujafanikiwa maishani lkn ifahamike kuwa mzazi wako anabaki kuwa mzazi.Bila mama baba hayupo,na wasipokuwepo hao hata wewe usingekuwepo.Tukumbuke tulikotoka,tuwakumbuke wazazi kwani wazazi wetu ndiyo mashujaa wetuUnapomjali mzazi nawe unabarikiwa,,,,Maandiko yanatuonya kwamba tuwaheshimu wazazi wetu ili tupate kuishi miaka mingi yenye kheri Duniani.

Jumamosi, 11 Machi 2017

MCHANA NA KATUNI

Enjoy

WEMA AJIUNGA CHADEMA RASMI

Hatimaye aliyewahi kuwa Miss Tanzania 2006 mrembo Wema Isack Sepetu ajiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema mapema juzi.Mrembo huyo awali alikuwa ni mwanachama wa chama cha Mapinduzi CCM ambapo itakumbukwa ktk uchaguzi wa mwaka juzi 2015 ambapo chama cha mapinduzi ndicho kilifanikiwa kutetea dola yeye alithubutu kugombea Ubunge kule Singida ingawa hakufanikiwa kupita ktk kura za maoni. Hata hvy pamoja na hiyo bado Wema alijitoa kwa hali na mali kuhakikisha CCM inashinda uchaguzi huo ambapo alizunguka nchi nzima akihamasisha vijana kuichagua CCM hasa wanawake huku akiwa na kampeni yake iloitwa,"MAMA SEMA NA MWANAO".Hata hvy chanzo chetu kinaeleza kuwa amepata mapokezi makubwa toka kwa viongozi na waumini was chama hicho pendwa(Chadema)na ambacho ndicho chama kikubwa cha upinzani nchini Tanzani. Wema anakuwa in mmoja kati ya watu maarufu na wanasiasa baadhi wakongwe na ambao kwa kipindi kifupi wameikacha CCM akiwemo aliyewahikuwa mshauri was rais was awamu zote mbili yaani ya tatu na ya nne Mh.Kingunge Ngombale Mwilu,lkn pia mawaziri wakuu wastaafu was awamu hizo Mh.Frederick T Sumaye na Mh.Edward Ngoyai Lowassa ambaye alikuja kuwa mgombea urais kupitia chama hicho na mwamvuli wa Umoja was Katiba ya Wananchi UKAWA. Nini kimemsibu ama kumsukuma Wema Sepetu kujiunga Chadema endelea kutufuatilia.

CCM YAWATEMA WASALITI

Chama cha mapinduzi CCM kimewatema ama kuwavua uanachama,uongozi sambamba na kuwapa onyo kali baadhi ya waliokuwa wanachama na viongozi wa ngazi mbalimbali ndani ya chama hicho kutokana na mapungufu mbalimbali waliokumbwa nayo ikiwemo usaliti,ukiukaji na uvunjaji wa sheria na maadili ya uongozi kwa mujibu wa katiba ya chama hicho tawala na kikongwe nchini Tanzania. Tiririka nayo hapa chini.