Jumamosi, 11 Machi 2017
WEMA AJIUNGA CHADEMA RASMI
Hatimaye aliyewahi kuwa Miss Tanzania 2006 mrembo Wema Isack Sepetu ajiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema mapema juzi.Mrembo huyo awali alikuwa ni mwanachama wa chama cha Mapinduzi CCM ambapo itakumbukwa ktk uchaguzi wa mwaka juzi 2015 ambapo chama cha mapinduzi ndicho kilifanikiwa kutetea dola yeye alithubutu kugombea Ubunge kule Singida ingawa hakufanikiwa kupita ktk kura za maoni.
Hata hvy pamoja na hiyo bado Wema alijitoa kwa hali na mali kuhakikisha CCM inashinda uchaguzi huo ambapo alizunguka nchi nzima akihamasisha vijana kuichagua CCM hasa wanawake huku akiwa na kampeni yake iloitwa,"MAMA SEMA NA MWANAO".Hata hvy chanzo chetu kinaeleza kuwa amepata mapokezi makubwa toka kwa viongozi na waumini was chama hicho pendwa(Chadema)na ambacho ndicho chama kikubwa cha upinzani nchini Tanzani.
Wema anakuwa in mmoja kati ya watu maarufu na wanasiasa baadhi wakongwe na ambao kwa kipindi kifupi wameikacha CCM akiwemo aliyewahikuwa mshauri was rais was awamu zote mbili yaani ya tatu na ya nne Mh.Kingunge Ngombale Mwilu,lkn pia mawaziri wakuu wastaafu was awamu hizo Mh.Frederick T Sumaye na Mh.Edward Ngoyai Lowassa ambaye alikuja kuwa mgombea urais kupitia chama hicho na mwamvuli wa Umoja was Katiba ya Wananchi UKAWA.
Nini kimemsibu ama kumsukuma Wema Sepetu kujiunga Chadema endelea kutufuatilia.

Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni