Ijumaa, 24 Machi 2017
MZAZI WAKO NDIYE SHUJA WAKO
Habari yako mpedwa msomaji wetu,karibu tena ktk ukurasa wetu huu adhimu unaolenga kutukumbusha kama jamii hasa vijana Duniani kote kwamba tufanye vyote vile lkn mwisho wa siku tuwakumbuke wazazi ama walezi wetu ambao walituzaa na kutulea kwa hali na mali na kutufanya tufike hapa tulipo leo.Haijalishi unayopitia,umefanikiwa ama hujafanikiwa maishani lkn ifahamike kuwa mzazi wako anabaki kuwa mzazi.Bila mama baba hayupo,na wasipokuwepo hao hata wewe usingekuwepo.Tukumbuke tulikotoka,tuwakumbuke wazazi kwani wazazi wetu ndiyo mashujaa wetuUnapomjali mzazi nawe unabarikiwa,,,,Maandiko yanatuonya kwamba tuwaheshimu wazazi wetu ili tupate kuishi miaka mingi yenye kheri Duniani.

Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni