Jumamosi, 9 Machi 2019

SIMBA FULL MZUKA KUMENYANA NA WAARABU WA JS SOURA USIKU HUU.

Mabingwa watetezi wa ligi kuu bara na wawakilishi pekee wa Tanzania katika ligi ya klabu bingwa Afrika timu ya Simba Sports Club iko mjini Soura nchini Algeria kumenyana vikali na timu ya JS Soura ya nchini humo katika mchezo wa marudiano ili kusaka pointi 3 muhimu za kuiwezesha kujiweka ktk nafasi nzuri ya kuingia hatua ya robo fainali za michuano hiyo mikubwa barani Afrika Kwa ngazi ya vilabu.

Simba wakiwa kundi D  linalojumuisha timu 4 za AS Vital ya Congo,Simba SC ya Tanzania,Al Ahaly ya Misri na JS Soura ya nchini Algeria wapikuwa wakishika nafasi ya pili kimsimamo katika kundi hilo gumu wakiwa na alama 6 kibindoni nyuma ya Al Ahaly ya Misri kabla ya mchezo uliyomalizika hivi punde kule mjini Kinshasa nchini Congo;mchezo ambao umemalizika Kwa vijana wa AS Vital kushinda Kwa mbinde goli 1-0 dhidi ya Al Ahaly.

Simba Kwa udi na uvumba watatakiwa kushinda mchezo huu ili kujiweka pazuri kabla ya kuja kumalizia mchezo ujao utakaopigwa jijini Dar Es Saalam dhidi ya AS Vital.

Kila lakheri Simba.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Simba.


Hakuna maoni: