Jumamosi, 9 Machi 2019

SIMBA HOI BIN TAABAN ALGERIA

Timu ya soka ya Simba SC ya jijini Dar es Saalam yashindwa kufurukuta ugegeni katika ligi ya Klabu Bingwa Afrika mbele ya JS Saoura ya nchini Algeria baada ya kukubali kichapo Cha magoli 2-0; mchezo uliyopigwa saa 4 usiku katika mji wa Saoura nchini Algeria.

Baada ya mchezo huo na ule uliyozikutanisha timu za AS Vita ya Congo dhidi ya Al Ahaly ya kutoka Misri ambapo mchezo ulimalizika Kwa timu ya AS Vita ikijikusanyia alama 3.

Havi Sasa msimamo wa kundi D uko hivi:-
(1)JS Saoura jumla alama 8
(2)AS Vita jumla alama 7
(3)Al Ahaly jumla alama 7
(4)Simba SC jumla alama 6.

Michezo itakayofuata itazikutanisha
(1)Al Ahaly Vs JS Saoura nchini Misri
(2)Simba SC Vs AS Vita nchini Tanzania; ambapo kivyovyote Simba itapaswa kushinda ili kuwa na matumani  ya kuingia hatua inayofuata ya robo fainali.

Hakuna maoni: